Usiku wa Jumapili, timu ya taifa ya
Spain ilishinda 2012 UEFA European Championsship, na wakawa timu ya
kwanza kushinda makombe matatu makubwa mfululizo. Spain kwanza
walishinda Euro 2008 na baadae World Cup 2010.
Ukiachana na hilo, wakati huo huo, Uchumi wa Spain umekuwa kwenye hali
mbaya sana. Wakati timu ya soka ikishinda ubingwa waulaya mambo yamezidi
kuwa mabaya kwa nchi hiyo hasa kwenye mgogoro wa kiuchumi wa madeni ya
nchi za ulaya.
Katika kutafuta namna atleast ya kupunguza deni la taifa, baadhi ya watu
na taasisi kadhaa zimekuja na habari za kufurahisha sana, kwa pamoja
wamekaa chini na kuanza kufanya tathmini ya thamani ya jumla ya
wachezaji wa kikosi cha wachezaji wa La Roja na namna gani thamani yao
inaweza kuisadia serikali ya Spain kukabiliana na matatizo ya kiuchumi
yanayoikabili.
Katika uchunguzi uliofanywa na CIA World Factbook, na
transfermarket.co.uk unaonyesha kwamba, ikiwa wachezaji wa Spain
watataifishwa na kuuzwa, basi uchumi wao kidogo utapata nafuu japo sio
sana.
Thamani ya kila mchezaji imefanyiwa tathmini kulingana na mikataba yao
ya hivi karibuni na soko la usajili lilivyo sasa - ambapo mtandao wa
transfermarkt.co.uk wamekadiria kwamba kikosi cha kwanza cha Spain
ambacho kinahusisha wachezaji bora kabisa duniani kina thamani ya ujumla
ya 400 million euros. Ukiwachanganya pamoja na walio benchi thamani
inapanda mpaka millioni 658 za uero, ambazo zinaweza kulipa asilimia
0.05 ya pato la taifa la Spain. Hivyo kuwauza wachezaji hawa kama
assests au kama dhamana inaweza kuwasaidia Spain kupunguza mzigo mkubwa
kwenye uchumi wake ikiwa serikali ingekuwa inaweza kutaifisha timu za
vilabu.
Kwa upana zaidi kwenye hili wazo lingekuwa na effect kubwa kwa vilabu
vikubwa viwili vya nchi hiyo. Spain ndio nyumbani kwa klabu mbili ambazo
ni moja ya vilabu maarufu zaidi duniani, F.C Barcelona na Rea Madrid
C.F. Hivi vilabu viwili ndio timu zinazokusanya wachezaji maarufu zaidi
duniani.
F.C Barcelona ndio nyumbanikwa mchezaji bora wa Euro 2012 - Andres
Iniesta na mchezaji bora wa dunia Lionel Messi. Kwa pamoja kikosi cha
Barca kina thamaniinayokadiriwa kufikia 603.5 million euros. Real Madrid
wapo nyuma ya maadui zao, kikosi chao kina thamani ya 546.5 millioni
euros, wakiwemo wachezaji kama Cristiano Ronaldo na Mesut Ozil. Pamoja,
wachezaji wa vilabu hivyo wana thamani ya ujumla inayokaribia 1.15
billion euro au asimilia 0.14 ya deni la Hispania.
HIZI NDIO THAMANI ZA BAADHI MCHEZAJI MUHIMU WA VILABU
• Cesc Fabregas: 50 million euros.
• Xavi Hernandez: 35 million euros.
• Andres Iniesta: 65 million euros.
• David Silva: 46 million euros.
• Xabi Alonso: 35 million euros.
• Iker Casillas: 35 million euros.
• Fernando Torres: 35 million euros. |
No comments:
Post a Comment