MCHAKATO UCHAGUZI DRFA KUANZA JULAI 15
Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeridhia
ombi la Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kuanza
mchakato wa uchaguzi wake Julai 15 mwaka huu.
DRFA
iliwasilisha ombi TFF ili kusogeza mbele kuanza kwa mchakato huo kwa
vile Katiba yao ambayo waliagizwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuifanyia
marekebisho kabla ya kuingia kwenye uchaguzi huo bado iko kwa Msajili.
Awali
DRFA ilikuwa ianze mchakato wa uchaguzi Julai Mosi mwaka huu. Kwa
mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, mchakato wa uchaguzi
unatakiwa kuchukua siku 40 tangu kuanza kutolewa fomu kwa wagombea hadi
siku yenyewe ya uchaguzi.
Pia
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imekubali ombi la Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Kigoma (KRFA) kuanza mapema mchakato wa uchaguzi wake. Sasa
mchakato wa uchaguzi wa chama hicho utaanza Septemba Mosi mwaka huu
badala ya Septemba 15 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali.
WAKENYA KUICHEZESHA NGORONGORO HEROES NYUMBANI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Kenya
kuchezesha mechi ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza Fainali za
Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Tanzania
(Ngorongoro Heroes) na Nigeria.
Mwamuzi
atakayechezesha mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itakayofanyika
Julai 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam atakuwa Moses
Ojwang Osano.
Waamuzi
wasaidizi watakuwa Peter Keireini na Elias Kuloba Wamalwa wakati
mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Thomas Onyango. Kamishna wa mechi
hiyo atakuwa Charles Masembe kutoka Uganda.
Pia
CAF imemteua Alfred Kishongole Rwiza wa Tanzania kuwa Kamishna wa
mechi ya michuano hiyo kati ya Misri na Kenya itakayochezwa jijini
Cairo kati ya Julai 27, 28 na 29 mwaka huu.
TEMEKE YAICHAPA DODOMA 2-0 COPA
Temeke
imefainikiwa kuilaza Dodoma mabao 2-0 katika mechi ya kundi C ya
michuano ya Copa Coca-Cola iliyochezwa leo (Julai 3 mwaka huu) kwenye
Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam.
Mabao
ya washindi ambao kwa matokeo hayo sasa wamefikisha pointi tano
yalifungwa dakika ya tano Hassan Kabunda wakati la pili lilifungwa
dakika ya 34 na Abdul Hassan.
Uwanja
wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam umeshuhudia Morogoro ikiibuka
na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Iringa lililofungwa dakika ya 37 na
Mutalemwa Katunzi.
Nayo
Kilimanjaro imeibuka na ushindi wa bao 1- dhidi ya Tabora katika mechi
iliyochezwa Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani. Bao hilo katika mechi hiyo
ya kundi D lilifungwa dakika ya 14 na Eric Christopher.
Kwa
matokeo hayo Tabora imebaki na pointi tatu baada ya kushinda mechi
moja tu dhidi ya Pwani, na imebakiza mechi moja dhidi ya Kusini Unguja
ambayo hata ikishinda haiwezi kuingia hatua ya 16 bora.
Nao
mabingwa watetezi Kigoma wamejiweka katika nafasi nzuri ya kucheza 16
bora baada ya kuitandika Kusini Pemba mabao 3-1 katika mchezo wa kundi A
uliochezwa Uwanja wa Tamco ulioko mkoani Pwani.
TIMU 10 TANZANIA KUCHEZA ROLLINGSTONE BURUNDI
Timu
10 za Tanzania Bara zitashiriki kwenye michuano ya Rollingstone kwa
vijana wenye umri chini ya miaka 20 ambayo mwaka huu itafanyika Makamba
nchini Burundi kuanzia Julai 7 mwaka huu.
Jumla
ya timu 24 zinashiriki mashindano hayo na zimepangwa katika makundi
sita tofauti. Timu nyingine zinatoka Burundi, Kenya, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC), Uganda na Zanzibar.
Timu
za Tanzania zilizoingia katika mashindano hayo ni Azam, Bishop High
School, Chakyi Academy, Coastal Union, Rollingstone, Ruvu Shooting,
Simba, TAYFA Academy, Yanga na Young Life.
Kwa
mujibu wa Katibu Mkuu wa Rollingstone, Issa Karata timu zote
zinatakiwa kwenda vyeti vya kuzaliwa vya wachezaji wake ili
kuthibitisha umri wao. Kamati ya Mashindano itakuwa na uamuzi wa mwisho
kuhusu umri wa mchezaji yeyote.
Kila
timu inatakiwa kuwa na wachezaji 20 na viongozi watano ambao
watagharamiwa na waandaaji kwa huduma za malazi na chakula kwa muda wote
wa mashindano hayo yaliyoanzishwa miaka 13 iliyopita.
|
No comments:
Post a Comment