Michuano ya Euro 2012 ilikuwa mizuri
sana labda uwe muitaliano, na baada ya kuangalia mataifa 16, mechi 31 na
magoli 76, Spain wakatawazwa kuwa mabingwa wa ulaya tena.
Wachezaji
kama Andres iniesta na Jordi Alba ambao walicheza vizuri sana kwenye
mchuano hiyo huku wakicheza kwenye kila mechi, lakini hawakuwa
wahispania hao pekee ambao waling'arahuko Poland na Ukraine.
Poland,
Russia, Sweden na Denmark wote waliichangamsha michuano hii kwenye
hatua ya makundi, lakini pia walikuwa na achezaji ambao walionyesha
viwango jinsi vilivyo hatari katika harakati za kusaidia mataifa yao.
Tukiwa
nalo hilo kichwani, na ufunguzi wa dirisha la usajili likifunguliwa,
hawa ni wachezaji watano - nje ya vikosi vilivyocheza fainali ambao
waliongeza thamani yao kwenye soko la usajili kupitia michuano ya Euro
2012.
ALAN DZAGOEV - KIUNGO MSHAMBULIAJI -URUSI
Akiwa
amefunga mabao matatu kwenye hatua za makundi, Alan Dzagoev
aljidhihirisha kuwa mmoja ya vijana wadogo wenye future nzuri kwenye
soka baada ya kuisadia Russia kupata ilichopta kwenye hatua ya makundi.
Dzagoev,
ambaye anaitumikia CSKA Moscow, alianza kufanya balaa kwenye mchezo wa
kwanza wa michuano hiyo akiiongoza Russia kuitandika Czech 4-1. Lakini
kwa bahati huo ndio ulikuwa ushindi wa mwisho kwa vijana hao kutoka
ulaya mashariki.
Alifunga kwenye mchezo dhidi ya Poland ambao
uliisha kwa sare ya 1-1 na kuonyesha kiwango kikubwa, alikuwa na control
kubwa ya mpira na jicho zuri la kupiga pasi kwenye michezo yote mitatu
Akiwa
amebakiza miezi sita kwenye mkataba wake, thamani yake kwenye soko la
usajili haitakuwa kubwa sana kwa sasa. CSKA watafanya kila kitu kuweza
kumfunga na mktaba wa muda mrefu.
Ikiwa watafanikiwa, wataweza
kupandisha thamani ya mchezaji huyo mpaka kufikia £12million. Ikiwa
watashindwa watamuuza kwa bei ya kawaida kuliko inavyopaswa kipindi
kijacho cha kiangazi.
THEODOR GEBRE SELASSIE - BEKI WA KULIA - CZECH
Czech
Republic walifika robo fainali za Euro, japokuwa walifungwa mabao 4-1
na Urusi, baada ya hapo wakaenda kuwafunga Ugiriki 2-1 na Poland 1-0.
Moja
ya sababu kubwa ya kuboreka kwa kiwango chao ilikuwa ni fomu nzuri ya
beki wao kulia Theodore Gebre Salassie, ambaye siku kadhaa kabla ya
michuano alikubali kuhamia Werder Bremen kutoka Slovan Liberec.
Inaonekana
ilikuwa faida kubwa kwa timu hiy ya Bundesiliga kukamilisha uhamisho wa
mchezaji huyo kabla ya michuano ya Euro 2012, wakiwa wamelipa
$1.6million kwa ajili ya kupata huduma za beki huyo mwenye kukaba na
kushambulia kwa kasi.
Kutokana kiwango chake alichokionyesha akiwa Czech, kwa hakika thamani yake ingekuwa imepanda zaidi ya aliyonunuliwa.
Kwa
kiwango alichonacho, nguvu na kuwa nautayari wa kusapoti mashambulizi
kwenye tatu ya mwisho - Gebre Selassie kwa sasa ana soko kubwa. Kwa
hakika akiendelea kuwa hivi alivyo Bremen watapata fedha nzuri sana kama
wataamua kumuuza.
ANDRIY YARMOLENKO - WINGA - UKRAINE Mfumo wa Ukraine wa kiufundi, ulikuwa ume-based. kwenye kushambulia zaidi, kupitia mawinga wao.
Huku
winga anyetumia mguu wa kushoto Andriy Yarmolenko akicheza upande wa
kulia na winga anayetumia mguu wa kushoto Yevhen Konoplyanka akicheza
winga ya kushoto, Ukraine mara kadhaa walikuwa wakiwatumia mawinga hawa
kwenye tatu ya mwisho kutengeneza mipira ya kupiga mashuti ya kupiga
krosi.
Huku wachezaji wengi kwa ujumla wakikosa kipaji cha
kuchezea mpira kulikuwa kizingiti cha Ukraine kusonga mbele, lakini
Yarmolenko, kipekee, alikuwa mchezaji aliyecheza vizuri sana ambaye
alionekana muda wowote angeweza kuwadhuru wapinzani.
Akiwa
mtulivu alikuwa akiingia katikati kupiga mashuti au kwenda pembeni
kuruhusu kutoa sapoti ya kulisha washambulaiji wa kati, Yarmolenko
alikuwa mzuri katika kumiliki mpirra na alikuwa mchezaji wa kwanza
wachezaji wenzie walikuwa wakimtafuta mara walipopata mpira ili aweze
kufanya utundu wake.
Yarmolenko kwa sasa anaichezea Dinamo Kyiv
kwenye nchi yake ya ukraine, ambapo huwa anachezeshwa katikati nyuma ya
mshambuliaji wa kati. Atakuwa na timu kibao zitakazowatuma mawakala
ikiwa taonyesha nia ya kuondoka kwenda kucheza nje ya mipaka ya nchi
hiyo.
Kyiv sasa watakuwa wakitegemea ada kubwa ya uhamisho baada ya kiwango alichoonyesha Euro.
JOAO MOUTINHO - KIUNO WA KATI - URENO Moja
kati ya wachezaji wachache kwenye michuano hii wenye uwezo wa kupiga
pasi vizuri tu kama ilivyo kwa viungo wa Spain, Joao Moutinho alikuwa
nyota iliyoangaza mafanikio ya Ureno kwenye Euro 2012, na ikiwa ataamua
kuhama kutoka klabu yake ya sasa ya Porto, atakuwa hajajitendea kitu
kibaya kwani kwa hakika atazivutia timu nying sana zenye majina makubwa.
Tofauti
na wachezaji wengine kwenye listi hii, Moutinho tayari alikuwa na bei
kubwa kabla ya michuano baada ya kucheza vizuri kwa misimu kadhaa akiwa
na Porto.
Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za vilabu vya
Uingereza Manchester United na Tottenham Hotspur zikiwania saini yake
kwenye soko la usajili la hivi sasa 0 huku thamani yake ikitajwa kufikia
paundi millioni 32 .
MATS HUMMELS - BEKI WAKATI - UJERUMANI Hatimaye
tumekutana na moja kati wachezaji walioifanya Ujerumani kuwa tishio
kwenye michuano ya Euro 2012 - huyu ni beki wa kati Mats Hummels.
Beki
huyo wa Borussia Dortmund amekuwa na michuano mizuri. Alizuia kwa
kiwango cha juu sana huku hali ya kuweza kuongoza safu ulinzi akionekana
kuwa nguvu na ufundi.
Ujerumani wakati wanaingia kwenye michuano
hii, safu ya ulinzi ndio iliyoonekana kuwa dhaifu, lakini chini ya
ulinzi wa Hummels, Ujerumani walionekana kubadilika na kuwa imara sana
kwenye safu ya ulinzi.
Amekuwa akionekana kuwa na thamani ya
£20million kwa sasa, Hummels hajaonyesha nia yoyote kuondoka Dortmund,
pia klabu yake haijaonyesha nia ya kumuuza.
Ukiangalia kiwango
chake kwenye Euro 2012, umri wake na potential aliyonayo huko mbeleni
inaonekana kipaji chake kitazidi kukuana kama ikiwa hivyo basi anaweza
kuja kuvunja rekodi ya usajili kwa mabeki ambayo kwa sasa inashikiliwana
Rio Ferdinand ambayo alisajiliwa na United kwa gharama ya £29million. |
No comments:
Post a Comment