PSI

PSI

Friday, July 6, 2012

KUTOKA KWA GEORGE BEST MPAKA CRISTIANO RONALDO - JEZI NO.7 YA MAN UNITED YAMUANGUKIA VALENCIA KUFUTA NYAYO ZA AKINA CANTONA AU AKINA OWEN?

Kwenye soka la dunia kuna jezi chache zilizo na historia kubwakuliko jezi namba 7 ya Manchester United, ikiwa imevaliwa na mastaa wakubwa sana walipokuwa pale Old Trafford, baada ya kuondoka kwa Micheal Owen sasa namba hiyo imeangukia kwenye umiliki wa Luis Antonio Valencia.

Tanguwakati wa msimu wake wa kwanza pale Theatre of Dreams, Raia huyu wa Ecuador amekuwa kipenzi cha mashabiki kwa sababu nyingi. ni mchezaji anayetoa mchango mkubwa sana kuchangia ushindi wa United, na nguvu na uwezo mkubwa kukaba.

Uamuzi wa kumpa mchezaji huyo wa Wigan jezi namba 7 utampa umaarufu zaidi Valencia   kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao wengi wamekuwa wakimpenda, wakati huo huo atakuwa na mzigo mkubwa wa kuweza kufuata nyayo za baadhi ya wachezaji wakubwa waliowahi kuivaa jezi hiyo.

Katika tukio hili kubwa kwa career ya Valencia - ebu tujikumbushe wachezaji waliong'ara na waliovurunda wakiwa wamevaa jezi namba saba kwenye kikosi cha Manchester United.

WALIOFANYA VIZURI NA JEZI NAMBA 7

ERIC CANTONA
'Mfalme Eric' ni mmoja kati ya wachezaji aliocheza kwa vipindi vifupi na kupata mafanikio wakiwa wamevaa jezi namba 7 ya Manchester United.

Cantona aliipokea jezi namba 7 kipindi cha kiangazi akiwasili kutokea Leeds United - uhamisho ambao ulileta maneno kwamba alikuja kuchukua nafasi ya Robson aliyekuwa akiendea mwishoni. Robson alibadilishiwa jezi na kupewa namba 12 na no.7 akachukua King Eric ambaye alikuja kufanya mambo makubwa sana akiwa na United - akiwasumbua mabeki kwa miaka mitano mpaka alipokuja kustaafu mwaka 1997.

Akitokea kutoka kwa mahasimu wakubwaLeeds, Cantona hakuchukua muda mrefu kuweza kupazoea Old Trafford. Kwa fomu aliyokuwa nayo Mark Hughes na Brian McClair pamoja na kuumia kwa Dion Dublin, kulimuhakikishia nafasi ya kucheza sana na kwa bahati nzuri akawa mchezaji wa kwanza kushinda taji la ligi kuu mara mbili mfululizo na klabu mbili tofauti.

Pamoja na mafaniko yake yote kwenye klabu hii, Cantona anakumbukwa sana kwa kitendo chake cha kumpiga shabiki wa Crystal Palace kwa staili ya kung-fu wakati alipotolewa nje kwa kadi nyekundu.

Cantona alifungiwa kwa miezi nane kucheza soka duniani kote huku akipigwa faini tofauti, na baadae akajaribu kuondoka United kwa mara kadhaa. lakini alibaki OT na kwenda kushinda makombe manne ya premier league, mawili ya FA na ngao tatu za hisani - pia alikuwa mchezaji bora namba tatu wa dunia mwaka 1993.

GEORGE BEST
Ingawa alikuwa anacheza sehemu moja kama ilivyo kwa Valencia - tofauti yao kubwa ni kwamba Best alikuwa maarufu zaidi kwa kuandikwa kwa mambo ya nje ya uwanja kuliko dimbani.

Alikuwa malaya mwenye kubadilisha wanawake kila kukicha huku akiwa mlevi namba moja, Best alikuwa kila siku kwenyekurasa za mbele za magazetikutokana na staili yake ya maisha, akiwa kwenye mahusiano na wasichana wa jumba la Playboy, kamari ulikuwa ndio mchezo wake huku akitumia vibaya fedha nyingi alizokuwa akipata kwenye manunuzi ya magari na vitu vingine vya anasa.

Pamoja na matukio yake yote uwanjani - Best alikuwa hatari dimbani. Alifanya mpira uonekane rahisi kucheza, akititirika kutoka winga ya kushoto na kuwapita mabeki shukrani kwa uwezo wake mkubwa wa kuchezea mpira na kasi. Lakini uwezo wake wa kuchezea miguu yote miwili ulimfanya atishe zaidi kwa kushindwa kutabirika - jambo ambalo lilimsaidia kufunga mabao mengi zaidi.

Wakati wa enzi za Best pale United, makombe waliyoshinda ni mataji mawili ya ligi na ngao mbili za hisani, wakati alimaliza kama mfungaji bora kwenye misimu sita mfululizo kabla ya kuondoka Old Trafford mwaka 1974 akiwa na miaka 27. Akaenda kuzichezea klabu nyingine 14 na hatimaye akastaafu mwaka 1984 na kufariki mwaka 2005 baada ya kuugua kwa muda mrefu matatizo ya ini.

BRYAN ROBSON
Hakukuwa na jambo kubwa ambalo Bryan Robson alishindwa kufanya, alikuwa mchezaji aliyekamilika na aliweza kuukabili mchezo na kuubadilisha huku akiongoza vizuri timu yake.

Maarufu zaidi kama nahodha aliyeitumikia kwa muda mrefu zaidi klabu hiyo kwenye historia, Robson alikuwa maarufu zaidi kwa kuwa kiungo ambaye alikuwa anafunga mabao mengi zaidi - lakini uwezo ake wa kukaba, stamina aliyonayo, na hali ya ushindani ilimfanya awe mchezaji wa aina yake.

Mwaka 1983 Robson alikuwa ndio nahodha wa kwanza kiingereza kubeba kombe la FA Cup kwa United, wakati mwaka uliofutia uhamisho wa kwenda Juventus nusra ukamilike. Ingawa aliendelea kubaki Old Trafford mpaka mwaka 1994, akiisaidia timu yake kubeba kombe la UEFA Cup mjini Rotterdam in 1991, kwa kuwafunga Barcelona kwenye fainali.

Akiitwa 'Nahodha mwenye maajabu', alicheza mechi 461 akiwa na United, akatia kambani magoli 99, huku mchezo wake wa mwisho dhidi ya Coventry City mwezi May 1994 uliisha kwa sare tasa. Amekuwa akisifiwa kwamba ni bora kuliko wote - kwa kura zilizopigwa na wachezaji wa zamani wa United mwaka 2011.

DAVID BECKHAM
Kama George Best alileta maisha ya ustaa kwa wanasoka, David Beckham alikuwa master wa maisha namna hiyo. Ndoa yake kwa muimbaji wa kundi la Spice Girls ndio ilikuwa moja ya chanzo kikubwa cha ustaa wake kukua, na kwa mujibu wa Sir Alex Ferguson suala la kuoa halikuwa zuri kwa avid Beckham.

Mapaparazi na wanahabari walikuwa wakimfuaa Beckham kila mahali alipokwenda huku kiungo huyo wa England akawa maarufu kupitiliza zaidi huku akifanya maajabu uwanjani - tukio la kukumbukwa zaidi ni lile goli alilofunga kati kati mwa uwanja dhidi ya West Ham mwaka 1996.

Beckham alianza kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza cha United kwenye msimu wa 1996-97 mpaka katikati mwa miaka ya 2000 alikuwa atayari ameshabeba makombe manne ya premier league, huku la tatu kati ya hayo likiwa la kukumbukwa zaidi kwa sababu lilikuwa ni moja kati ya matatu waliyobeba United mwaka 1999

 CRISTIANO RONALDO
Mchezaji wa kwanza wa kireno kuichezea United, akiwa amesajiliwa haraka baada ya David Beckham kuondoka kwenda Madrid.

Usajili wake uliogharimu United paundi millioni 12 uliwashangaza washabiki wengi wa United, lakini dakika 30 alizocheza kwenye mechi dhidi ya Bolton ambayo United walishinda kwa 4-0 - ziliwapa majibu yote waliyohitaji kuhusu bei yake.

 Pamoja na kuanza kucheza kibafsi zaidi kwenye miaka yake miwili ya kwanza akiwa United, lakini aliimarika kiakili na kimwili na kuanza kuisadia klabu yake kuanza kukusanya mataji kama lilivyo ada. Ronaldo akishirikiana na wachezaji wenzie kama akina Wayne Rooney waliiwezesha United kushinda makombe matatu ya premier league, kombe la klabu bingwa ya ulaya na dunia, pamoja na makombe mengine manne tofauti - huku Ronaldo akifunga mabao 127 huku akitoa assits nyingi zilizochangia mafanikio makubwa kwa Manchester United.
Mafanikio ya Ronaldo akiwa na United hayakuhusiana na timu tu baada ya kuwa mchezaji wa kwanza premier league kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa dunia wa FIFA, na mchezaji wa kwanza wa United kushinda Ballon d'Or tangu Best alivyoshinda mwaka 1968.

Ronaldo akiuja kuwaachia huzuni mkubwa mashabiki wa United baada ya kufuata nyayo za Beckham  kujiunga na Real Madrid mwezi June 2009 baada ya Real kulipa ada ya uhamisho iliyoweka rekodi ya dunia ya paundi millioni 80.
 
WALIOVULUNDA
MICHEAL OWEN
Kutoka siku ya kwanza Micheal Owen alikuwa akipigania nafasi ya kuwa mchezaji anayeanza kwenye kikosi cha kwanza cha United. Ukweli wa kwamba tayari alishakuwa akifikiriwa kwamba ni gwiji wa soka wa Liverpool lilikuwa tatizo la kwanza, lakini pia kushindania namba na Wayen Rooney na Dimitar Berbatov.

Majeruhi pia yalikuwa ndio kikwazo kikuu kwa Owen akiwa na United. Kuibuka kwa Danny Welbeck na Federico Macheda pia kukatishia uwepo wa mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid, ingawa goli la dakika za majeruhi dhidi ya Man City pale Old Trafford litamfanya akumbukwe sana mashtani wekundu.

Pia alikuwa nyota wa mchezo kwenye mechi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Wolfsburg ,wezi December 2009 baada ya kufunga mabao matatu muhimu, ingawa majeruhi yaliendelea kumuandama msimu huo wote na akakosa miezi mitatu ya msimu.

Kwenye msimu wa pili akiwa na United alishinda medali yake ya kwanza ya premier league akicheza mechi 11 tu. Ingawa msimu uliopita Owen alicheza mechi moja tu kwa msimu mzima, na hatimaye United wakaamua kutomuongezea mkataba mpyana huo ndio ukawa mwisho wa wake na United.

Owen anawakilisha kundi la wachezaji wanne waliovaa jezi namba 7 kwa united ambao walivurunda wakiwemo wafuatao.

WALIOCHEMSHA WAKIWA WAMEVAA JEZI NO.7
1 - Micheal Owen

2 - Ralph Milne

3 - Keith Gillespie

4 - Ashley Grimes

No comments: