Anton Ferdinand ameieleza mahakama siku ya Jumatatu
kwamba 'ningelikerwa sana' na matamshi ya ubaguzi wa rangi kama
ningelimsikia John Terry akitamka maneno hayo.
John Terry, mwenye umri wa miaka 31, na ambaye
ni mchezaji soka wa Chelsea na vile vile timu ya taifa ya England,
anashtakiwa kwa madai kwamba alimtukana Anton Ferdinand, kwa kutumia
lugha ya ubaguzi wa rangi katika mechi uwanjani, madai ambayo John Terry
ameyakanusha.
Inadaiwa
Terry, nahodha wa timu ya Chelsea, alitamka maneno hayo dhidi ya mlinzi
wa QPR, wakati timu hizo zilipopambana katika uwanja wa QPR wa barabara
ya Loftus, mwezi Oktoba.
Kesi hiyo inatazamiwa itaendelea kwa siku tano katika mahakama ya Westminster, mjini London.
Ikiwa Terry atapatikana na hatia, hukumu kali zaidi itakuwa ni kutozwa faini ya pauni 2,500.
Ferdinand alisema mahakamani kwamba "wakati mtu
anapoleta suala la rangi katika mchezo, huwa amezidisha matusi na
kuyafikisha hatua nyingine".
Inadaiwa kwamba mlinzi huyo wa Chelsea alimuita mwenzake mweusi, na akitumia maneno pia yaliyohusishwa na ngono.
Mtaalamu wa lugha ya kutafsiri yaliyosema kwa
kuangalia mdomo, Susan Whitewood, alithibitisha kwamba matamshi
yasiyofaa yalitumiwa na Terry.
Ferdinand aliielezea mahakama kwamba awali hakudhani lugha ya ubaguzi wa rangi ilitumika.
Lakini baada ya mechi, rafiki yake wa kike
alimchezea video iliyokuwa katika tovuti ya YouTube, na baada ya hapo,
alibadilisha nia na kuamua kuchukua hatua za kisheria.
Ferdinand alisema kwamba kama moja kwa moja
angelitambua Terry alimtukana uwanjani kwa kutumia matamshi hayo, basi
papo hapo angeliwaarifu maafisa waliyosimamia mechi hiyo. |
No comments:
Post a Comment