Akiwa ameishi kwenye kivuli cha Lionel
Messi kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, labda mwaka 2012 ni nafasi
nzuri zaidi kwa Cristiano Ronaldo kuvunja utawala wa 'mchawi wa
Kiargentina' na kurudisha kwenye himaya yake tuzo ya mwanasoka bora wa
dunia.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid alipoteza utawala wa tuzo ya mchezaji
bora wa dunia tangu mwaka 2009 na kiukweli hajaonekana kama atakuja
kuishinda tena tuzo tangu Messi aanze kufanya maajabu huku kikosi chake
cha Barcelona kikitawala La Liga na mpaka nje ya mipaka ya Spain.
Lakini mwaka huu, kwa kuangalia mafanikio aliyoyapata Mreno huyu na kuwa
na mafanikio finyu kwa Messi kutampa Ronaldo tumaini kwa mara nyingine
tena kutajwa kuwa mchezaji bora na kunyakua Ballon d'Or.
Ronaldo alinunuliwa kwa ada ya uhamisho ya £80million iliyovunja rekodi
kutoka Manchester United kwenda Real Madrid - huku akionekana tumaini
jipya katikakurudisha siku nzuri kwa Los Blancos, lakini kwa bahati
mbaya aliwasili Santiago Bernebau wakati ndege ya mafanikio ya kikosi
cha Barcelona chini ya Pep Guardiola ndio ikianza kushika kasi kuruka.
Lakini hatimaye baada ya miaka mitatu na kufuatia kuongezeka kwa
Mourinho kwenye timu ya Madrid, kila kitu kimeanza kurudi kwenye nafasi
kwa Madrid na Ronaldo binafsi.
Ronaldo bila ubishi wala shaka ndio alikuwa star wa Real Madrid msimu
uliopita huku wakishinda La Liga kwa pointi 100, tisa zaidi ya Barcelona
na kuvunja rekodi waliyoiweka wenyewe kwa kuchukua ubingwa huku wakiwa
na pointi 99.
Mreno anayevaa jezi namba 7 mgongoni alifunga mabao 46 kwenye ligi hiyo -
zaidi ya nusu ya mabao aliyokuwa nayo mchezaji wa pili anayemfuatia kwa
wachezaji wa Madrid - Gonzalo Higuain aliyetia kambani magoli 22.
Mafanikio haya pia yakafunikwa na kivuli cha Messi, baada ya Muargentina huyo kutupia mabao 50 kwenye la liga.
Barani ulaya pia, Ronaldo alicheza kwa kiwango kikubwa. Alifunga magoli
10 kwenye mechi 10 za Champions league huku Real wakitolewa kwenye nusu
fainali kwa penati na Bayern Munich. Lakini kwa bahati mbaya tena
pamoja na kucheza vizuri, Ronaldo alimaliza nyuma ya Mario Gomez
aliyekuwa na magoli 12 - huku kwa mara nyingine tena Messi alikuwa juu
yake kwa kumaliza kama mfungaji bora wa michuano hiyo kwa mara tatu
mfululizo hiyo akiwa na mabao 14.
Hata baada ya msimu kuisha, Ronaldo bado alikuwa na nafasi nyingine ya
kushindana ambayo Messi hakuweza kushindania: alikuwa na michuano ya
kimataifa iliyokuwa njiani. Kuiongoza nchi yake ya Ureno kwenye michuano
mikubwa ya Euro 2012.
Kufanya vizuri kwenye michuano hii kungemuhakikishia nafasi kubwa Ronaldo kushinda Ballon d'Or dhidi ya Messi.
Kwa bahati mbaya akaanza vibaya michuano hii kwa Ureno kufungwa na
Ujerumani, kabla ya kucheza vibaya na kukosa nafasi nyingi za kufnga
kwenye mchezo wa pili wa kundi la kifo dhidi ya Denmark, lakini wale
wanaompinga Ronaldo aliwanyamazisha kwenye mchezo wa lazima kushinda na
mwisho wa makundi dhidi ya timu ya Uholanzi. Mwanaume huyu alifunga
mabao mawili ya ushindi huku akicheza kwa kiwango cha juu na kupelekea
timu yake kuvuka kwa ushindi 2-1. Pia aliendeleza balaa kwenye mchezo wa
robo fainali dhidi ya Czeh Republic kwa kufunga goli la ushindi na
kuipeleka Ureno nusu fainali.
Ingawa, pamoja na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyepiga mashuti mengi
kwenye lango la adui, na kumaliza akiwa amefunga mabao matatu sawa na
mfungaji bora wa michuano hiyo Fernando Torres, Ronaldo atakumbukwa
zaidi kwa michuano hii baada ya kushindwa kupiga penati ya mwisho kwenye
mechi ya nusu fainali dhidi ya Spain.Ronaldo na kocha wake Paul Bento
walicheza kamari ya kusubiri kupiga penati ya mwishodhidi ya Spain,
lakini baada ya Moutinho na Bruno Alves kushindwa kufunga - Spain
wakaimaliza mechi kabla ya Ronaldo hajapiga nafasi ya kupiga penati yake
ya mwisho.
Mapema mwezi June, Messi - ambaye bado hajaonyesha kiwango chake cha
klabu kwenye timu ya taifa - alicheza kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya
Brazil. Inaweza ikawa kweli ilikuwa mechi ya kirafiki, lakini kiwango
alichoonyesha Messi kwa kufunga hat trick lilikuwa jambo la kukumbukwa.
Goli la tatu la Messi litakumbukwa zaidi, alitoka nyuma na kuwapita
mabeki kadhaa kisha kufunga kwa mkwaju mkali kulipelekea idadi ya jumla
ya magoli yake kwa msimu 2011-2012 kufikia 82. Idadi ya kutisha sana.
Ronaldo anaweza akawa akashinda kikombe kikubwa kuliko Messi 2012,
lakini atahitaji kucheza kwa kiwango chake kwa asilimia 100 na
ku-deliver katika kipindi cha nusu mwaka kilichobaki ikiwa anataka
kujihakikishia ushindi wa Ballon d'Or inayotolewa mwezi Desemba. |
No comments:
Post a Comment