WASHAMCHOKA! Manchester City ipo tayari kusikiliza ofa kutoka timu
yoyote ile ambayo itaonesha nia ya kumtwaa mchezaji wao, Kolo Toure.Wakati Manchester City wakionesha nia ya kumuuza, tayari timu ya
Bursaspor ya Uturuki inaonekana ipo tayari kumtwaa beki huyo wa kati wa
kimataifa wa Ivory Coast.
Manchester City inaonekana haitaki kupata hasara na kuamua kumuuza
mchezaji huyo mapema, ambaye amebakisha mkataba wa mwaka mmoja ndani ya
Etihad.
Mbali na timu hiyo ya Uturuki, pia klabu kadhaa za Mashariki ya Kati
zimeonesha nia ya kumtwaa mchezaji huyo anayefikia ukingoni katika
maisha yake ya soka.
Toure, 31, alijikuta katika wakati mgumu katika kikosi cha Roberto
Mancini wakati yeye pamoja na Vincent Kompany na Joleon Lescott kuumia.
Manchester City imesisitiza haitaki kuona mchezaji huyo anaondoka bure, ndio maana inaamua kumuuza mapema. |
No comments:
Post a Comment