KITUO cha runinga cha SuperSport ambacho kipo ndani ya king’amuzi cha
DStv ambacho kinaonyesha michuano ya Kombe la Kagame 2012, kimekuwa
kikirusha matangazo ya michuano hiyo kwa lugha ya Kiswahili. Michuano hiyo ambayo inaandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) imekuwa ikiendelea kufanyika kwenye Uwanja wa Taifa na Chamazi jijini Dar, imeonekana kuteka hisia za watu wengi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Ofisa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi amesema SuperSport itaonyesha michuano yote moja kwa moja kuanzia ilipoanza Julai 14 mpaka Julai 28 ambapo wachambuzi wa soka, Florian Kaijage, Clifford Ndimbo na Michael Were wamekuwa wakifanya uchambuzi katika lugha ya Kiswahili. Matangazo hayo ya michuano hiyo yanapatikana katika SuperSport 9, kwa anayehitaji kusikiliza matangazo kwa Kiswahili anatakiwa kuchagua kupitia rimoti yake kwa kuwa pia kuna matangazo ya Kiingereza yanayopatikana kupitia kituo hichohicho. |
PSI
Wednesday, July 18, 2012
Kombe la Kagame latangazwa SuperSport kwa Kiswahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment