Stiker wa Napoli Edinson Cavani amesema kama Club ya Chelsea
inamtaka itabidi imlipe mshahara mkubwa kama wanavyolipwa wachezaji
wengine wakubwa ambapo mkali huyu mwenye umri wa miaka 25 anapewa nafasi
ya kuchukua namba ya Drogba na atakubali kusain kama Chelsea watakubali
kumlipa bilioni 770 za Kitanzania.
Gazeti la Uingereza la Daily Mail, Cavani anataka alipwe
mshahara unaofanana na John Terry, Lampard na Torres ambao wote
wanachukua zaidi ya pound laki moja na nusu kwa wiki ambayo ni zaidi ya
bilioni 3 na nusu kwa noti ya kibongo.
Cavani amekua akihusishwa kuhamia Chelsea for some time, kama
haufahamu, nakupa hii kwamba Cavani kwenye msimu uliopita wakati
akiichezea Napoli, alifunga magoli 94 ndani ya mechi 66 ndio maana
inaaminika kwamba anaweza kuliziba pengo la Drogba vizuri, hiyo hapo
chini ni video ya magoli ambayo Edinson amewahi kufunga. |
No comments:
Post a Comment