MABINGWA watetezi wa Klabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati Kombe la Kagame, Yanga jana wamefufua
matumaini ya kutetea taji lao, baada ya kuitandika Waw Salaam ya Sudan
Kusini magoli 7-1 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam katika mchezo wa
Kundi C.
Nyota wa mchezo wa jana,
alikuwa ni Mwanasoka Bora wa Uganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ aliyeifungia
timu yake mabao matatu na kuondoka na mpira, Kiiza anayeingia msimu wa
pili Yanga, alitikisa nyavu katika dakika za 19, 27 na 30, wakati Said
Bahanuzi alifunga dakika za 15 na 17, Stefano Mwasyika dakika ya 25 na
mwisho Nizar Khalfan dakika ya 75.
Klabu ya Sudan Kusini, taifa
linaloshiriki kwa mara ya kwanza michuano hii, ilipata bao la kufutia
machozi dakika ya 88, mfungaji Hamisi Bashama. Katika mchezo wa kundi
hilo, C uliotangulia, Atleltico ya Burndi ilitoka sare ya bila kufungana
na APR ya Rwanda.
APR na Atletico
zimejihakikishia kuingia Roo Fainali, wakati Yanga unaweza kusema kwa
asilimia 90 imeshafuzu nayo, kwani ili isivuke, Waw Salam wanatakiwa
kuifunga Atletico zaidi ya mabao 7-0. (Stori imeandikwa na
bongostaz.blogspot.com)
|
No comments:
Post a Comment