PSI

PSI

Tuesday, July 17, 2012

MANCHESTER UNITED YAONGOZA TENA KWA TIMU YA MICHEZO YENYE THAMANI KUBWA ZAIDI DUNIANI

Jarida maarufu la kimarekani la Forbes leo hii limetoa tena listi ya vilabu vya michezo yote vyenye thamani kubwa duniani, na kwa mara nyingine tena pamoja na kutochukua kombe lolote msimu uliopita na kutolewa mapema kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya Manchester United imeendelea kushika usukani mwa vilabu tajiri duniani huku ikifuatiwa na Real Madrid. 

Timu nyingine za mchezo wa soka zilizopo kwenye Top 10 ni Barcelona wanaoshika nafasi ya nane, huku Arsenal ya England ambayo haijchukua kombe lolote kwa miaka inayokaribia kufikia nane ikishika nafasi ya 10, wakiwazidi mabingwa wapya wa Ulaya Chelsea wanaoshika nafasi ya 45 huku matajiri wa England Man City wakiwa hawapo hata kwenye Top 50. Timu nyingine za soka zilizopo kwenye listi hiyo ni Bayern Munich wanashika nafasi ya 11, AC Milan wanashika nafasi ya 27.
#1 Manchester United ($2.23 billion)
#3 New York Yankees ($1.85 billion)
#5 Washington Redskins ($1.56 billion)
#6 New England Patriots ($1.4 billion)
#9 New York Giants ($1.3 billion)


No comments: