Serena Williams kutoka Marekani amemshinda Agnieszka
Radwanska wa Poland 6-1 5-7 6-2 kujishindia taji la wanawake la
mashindano ya kila mwaka ya Wimbledon.
Hii ni mara ya tano kwa Serena kushinda
mashindano haya, ikiwa ni mara yake ya 14 kushinda mashindano ya kiwango
kikubwa kama hiki(Grand slam).
Serena
alianza vizuri kwa kitisho seti ya kwanza akionyesha dalila za kumaliza
kazi kwa haraka alipomchapa Radwanska 6-1 seti ya kwanza iliyomalizika
kwa mda mfupi kuliko ilivyotarajiwa.
Hata hivyo mambo yalibadilika katika seti ya
pili wachezaji hawa waliporejea baada ya kukwepa mvua iliyosababisha
mechi kusimama kwa mda wa dakika 25 .
Radwanska alianza kuonyesha dalili za kurejea na kujiamini kuweza
kunyakua ushindi kutoka kwa mkongwe wa mashindano haya na kuondoka na
ushindi wa seti ya pili 7-5.
Seti ya tatu ilipoanza, Serena lionyesha ukomavu
wake na uzowefu kwa kumdhibiti mpinzani na kutumia kila mbinu alizo
nazo akiweka rekodi ya ''ace'' kupiga mashuti ya mpira bila kuguswa, na
sasa ametimiza 'ace' 100 akimpita Philipp Kohlschreiber wa Ujerumani
ambaye anashikilia rekodi ya ace 98.
Kabla ya pambano la leo Serena alikua na jumla
ya 'ace' 85, kwa hiyo katika mechi ya leo ametumia ace'15 kuweza kumpiku
raia wa Poland.
Hivyo ndivyo Serena alivyoweza kuuchangamsha
uwanja wa Wimbledon na kunyanyua ngao ya 'rosewater dish' inayowaniwa na
wanawake kwenye uwanja wa Wimbledon kila mwaka.
|
No comments:
Post a Comment