Aaron Ramsey akifunga bao juzi dhidi ya Korea ya kusini
Jamani huu ni mkosi au ni bahati mbaya tu inatokea?
Kila mchezaji wa Arsenal Aaron Ramsey
anapofunga bao basi masaa kadhaa baadae kuna kifo cha mtu maarufu
kinatokea. Hii ilianza wakati alipofunga bao dhidi ya Sunderland na
masaa 24 baadae mwanamuziki Whitney Houstona akafariki dunia, na pale
alipofunga goli la ushindi ya Manchester United - majeshi ya Marekani
yakamuua Osama Bin Laden, Ramsey alipowatungua Tottenhm, mbunifu,
mmiliki na aliyekuwa CEO wa kampuni inayotengeneza bidhaa za Apple ya
Marekani akafariki dunia, na tena alipowafunga Marseille kwenye
Champions league - Colonel Maamar Gaddafi akauwawa na majeshi ya waasi
nchini kwake Libya. | | | |
No comments:
Post a Comment