Fifa imeanzisha uchunguzi
kubaini ukweli wa madai ya mchezaji wa Manchester City kuwa alidhulumiwa
kutokana na rangi yake timu hiyo ilipokuwa Croatia.
Shirikisho hilo la soka duniani linaendeleza
uchunguzi huo kufuatia madai ya Seko Fofana, 20, kuwa alidhihakiwa
walipokuwa wakishiriki mechi ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21.
Wakati huohuo shirikisho hilo
limeiagiza shirikisho la soka la Italia kuanzisha uchunguzi dhidi ya
,Carlo Tavecchio ambaye anatuhumiwa kwa kutamka maneno ya kuwadunisha
wachezaji wenye asili ya Afrika.
Msemaji wa FIFA ameiambia BBC kuwa wanakusudia
kutafuta suluhu ya tukio lililompelekea kocha wa City Patrick Vieira
kuwaondoa wachezaji wake uwanjani.
Kwa upande wake shirikisho la kandanda la Croatia limeanzisha uchunguzi wake.
Msemaji huyo alisema kuwa mwenyekiti wa jopo la
kuchunguza dhulma kwa misingi ya rangi Jeffrey Webb anafuatilia kwa
karibu matukio hayo.
No comments:
Post a Comment