Kiungo wa Arsenal amesema
anajutia kitendo chake cha kupigwa picha akivuta sigara hadharani katika
bwawa la kuogelea huko Las Vegas.
Wilshere mwenye miaka 22 amelaumiwa hasa kwa
kuzingatia wakati picha hizo ziliposambaa timu yake ya Uingereza ilikuwa
katika kipindi kigumu ikitolewa katika Kombe la Dunia hatua za mwanzo.
Hii ni mara ya pili Wilshere kufumwa akivuta sigara katika kipindi cha miezi tisa.
Mwezi wa kumi, Wilshere alipigwa picha akivuta sigara akiwa nje ya Klabu ya Usiku baada ya kuishinda Napoli.
"Ninajutia," alisema. "haikubaliki na nitakubaliana na matokeo kisha maisha yataendelea."
Meneja Arsenal, Arsene Wenger alimkosoa Wilshere na akasema ataongea nae kuhusu suala hili.
No comments:
Post a Comment