PSI

PSI

Monday, January 19, 2015

Aubameyang,aahidi kung'ara AFCON 2015

Pierre-Emerick Aubameyang
Nahodha wa timu ya Gabon Pierre-Emerick Aubameyang ameweka wazi matamanio yake ya kuwa miongoni mwa wakali watakao weka historia ya uchezaji mahiri katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu 2015.
Baada ya kuweka kimiani magoli 2-0 walipokwaana na Burjina Faso siku ya Jumamosi,alisema alijaribu kucheza kadiri ya kiwango chake na kujifananisha na Didier Drogba ama Samuel Eto’o.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na tano anataka kuwapa Imani washabiki wake wanaotegemea mambo mazuri uwanjani, Pierre-Emerick Aubameyang anaichezea timu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund ameanza vyema michuano mikubwa barani Africa
Aubameyang amesawazisha hat-trick kwenye mpira wa adhabu wakati Gabon iliposhinda 4-1 kwenye michuano ya kombe la dunia na kuwashinda Niger.
Alijiwekea rekodi nzuri ya kung’ara pale aliposawazisha baada ya dakika ya kumi na nane ya mchezo na akahusika kutengeneza uzaliwaji wa goli la pili na mpira ukakakwamishwa kimiani na Malick Evouna katika kipindi cha pili.
Kwa namna ya tofauti kabisa tena isivyo kawaida kwa Aubameyang katika michuano ya mwaka 2012,ambayo ilichezwa baina ya Gabon na Equatorial Guinea, ni hapo ambapo alifanya kosa ambalo halisahau asilani aliposhindwa kumalizia vyema mpira wa adhabu katika mchezo wa nusu fainali akatoa boko na Mali wakaibuka kidedea.
Mwenyewe anajitetea kuwa, usipokosea huwezi kujipima uwezo wako,penati dhidi ya Mali katika nusu fainali ,hata kama niliikosa,inabaki kuwa kumbukumbu njema maishani mwangu kwasababu imenifanya kipaji changu kikue mara dufu.
Kwa michuano hii ya mataifa ya Afrika ndo tunaanzia chini,ni michuano mipya,na imeanza vyema kwangu kukwamisha mpira kimiani.Naamini mara hii tena tutatinga nusu fainali,na tukipata penati ingine tena, sitafanya makosa,nitafunga

No comments: