PSI

PSI

Wednesday, January 10, 2018

Droo Kombe la FA: Manchester United wapewa Yeovil Town

 Yeovil Town v Manchester United in 2015
Klabu ya Yeovil Town inayocheza ligi ya daraja la tatu, ambayo ndiyo klabu ya ngazi ya chini zaidi iliyosalia katika Kombe la FA msimu huu, imepangwa kukutana na mabingwa mara 12 wa kombe hilo Manchester United raundi ya nne.
Tottenham pia watakutana na klabu ya League Two, Newport County.
Viongozi wa Ligi ya Premia Manchester City wamepangwa kukutana na mshindi kati ya Cardiff City na Mansfield.
Nottingham Forest, ambao waliwaondoa mabingwa watetezi Arsenal Jumapili watakutana na wenzao wa ligi ya Championship Hull City.
Mechi za raundi ya nne zitachezwa wikendi ya 26-29 Januari.

Darren Way (centre)
Droo kamili raundi ya nne:
Liverpool v West Brom
Peterborough v Fleetwood/Leicester
Huddersfield v Birmingham
Notts County v Wolves/Swansea
Yeovil v Manchester United
Carlisle/Sheffield Wednesday v Stevenage/Reading
Cardiff/Mansfield v Manchester City
MK Dons v Coventry
Millwall v Rochdale
Southampton v Watford
Middlesbrough v Brighton/Crystal Palace
Bournemouth/Wigan v Shrewsbury/West Ham
Hull v Nottingham Forest
Newport County v Tottenham
Norwich/Chelsea v Newcastle
Sheffield United v Preston

No comments: