Fabio Capello jana usiku
amemtupia vijembe Wayne Rooney na kumlaumu mshambuliaji huyo wa
Manchester United kwa England kutolewa mapema kwenye Euro 2012.
Kocha huyo wa zamani wa Three Lions alikasirishwa na maoni ya Rooney
kwamba ufundishaji wake kwa wachezaji ulikuwa una shida kuwafikia
wachezaji kwa sababu ya lugha kwa kuwa muitaliano huyo hakuwa muongeaji
mzuri wa kiingereza.
Lakini baada ya Roy Hodgson kukiri kwamba kwamba kiwango cha Rooney
kwenye robo fainali dhidi ya Italia kilichangia kwa kiasi kikubwa
England kutolewa mapema na sasa Capello nae kapata kwa kusemea.
"Baada ya kuangalia mchezo wa England dhidi ya Italia nafikiri Rooney anaelewa ki-scotland pekee," alisema Capello.
"Hilo ni kwa sababu anacheza vizuri akiwa na Manchester United tu,
mahala anapofundishwa na Sir Alex Ferguson ambaye anaongea kiscottish."
|
No comments:
Post a Comment