PSI

PSI

Monday, June 11, 2012

ITALIA YAIBANA HISPANIA


Mabingwa wa Dunia Uhispania imeanza utetezi wa Kombe lao la ubingwa wa mashindano ya Ulaya kwa sare ya 1-1 dhidi ya Italia katika pambano la kundi C mjini Gdansk.
Italia ndiyo iliyotangulia baada ya kipindi cha kwanza kumalizika bila bao lolote kufungwa na alikua Antonio Di Natale aliyeingia badala ya Balloteli kufunga bao katika dakika ya 60.
Dakika nne baadaye Mabingwa wa Dunia na Ulaya walifumania lango la Italia na licha ya juhudi na umahiri wa Mabeki David Silva alimuona Cesc Fabregas na kumuwekea pasi maridhawa na bila kufanya makosa akaupenyeza mpira kumpita goli wa Italia Buffon.
Italia yachacha na Uhispania
Matokeo hayo yanaliweka kundi la C wazi ambapo Italia na Uhispania zinaondoka zote zikiwa na pointi moja

No comments: