Baada ya siku chache zilizopita
website hii ilikuwa ya kwanza kuripoti kwamba klabu ya Yanga ipo katika
hatua za mwisho za kumsaini Marcio Maximo, leo hii imefahamika kwamba
kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa 'Taifa Stars' Mbrazil, Marcio
Maximo anatarajia kutua nchini kwa mara nyingine tena toka aondoke
nchini mwezi juni mwaka 2010 siku ya jumapili juni 17 saa 9 alasiri.
Maximo anakuja nchini kuchukua mikoba ya Mserbia wa Yanga Kostadin Papic
aliyenyimwa mkataba mpya, baada ya ule wa awali wa miezi 6 kuisha
wakati ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2011/12 ukielekea mwishoni.
Maximo awali alitarajiwa awasili nchini hapo kesho, na kwa mujibu wa
taarifa rasmi na zinasema kocha huyo mwenye msimamo mkali atawasili
jumapili na shirika la ndege ya Emirates
|
No comments:
Post a Comment