PSI

PSI

Friday, August 31, 2012

Azam FC yaleta straika kutoka Congo

AZAM FC imefanikiwa kupata mrithi wa kiungo wao waliyemtimua, George Odhiambo ‘Blackberry’, baada ya kumnasa mshambuliaji kutoka DR Congo aliyefahamika kwa jina la Papii.

Odhiambo alitimuliwa wiki iliyopita kutokana na utovu wa nidhamu uliotokana na kutohudhuria mazoezi kwa muda wa siku nne mfululizo.

Kwa mujibu wa kiongozi mmoja kutoka katika benchi la ufundi la timu hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa kuwa si msemaji wa timu, alisema mchezaji huyo aliyemfahamu kwa jina moja la Papii, alianza mazoezi tangu wiki iliyopita.

Amesema kuwa amekuwa akionyesha uwezo mkubwa mazoezini hasa katika kupachika mabao. “Kuna mchezaji mpya kaja na ana wiki sasa anafanya mazoezi, namfahamu kwa jina moja
tu la Papii na ametoka Congo, hucheza nafasi ya ushambuliaji

No comments: