Simba ilianza kuweka rekodi hiyo ilipotwaa Kombe la Ligi Kuu Tanzania
Bara, ilipoanzishwa mwaka 1967, wakati huo klabu hiyo ilikuwa
ikijulikana kama Sunderland. Wekundu hao wakaendelea kwa kunyakua
Kombe la Kagame, mara baada ya michuano hiyo kuanzishwa mwaka 1974 na
kufanya hivyo tena katika lile la Tusker lililoanza 2002, kombe ambalo
walilinyakua mara tatu mfululizo tangu lianzishwe. Mabingwa hao
watetezi wa Ligi Kuu ya Bara, mwaka huu waliendeleza ubabe huo katika
michuano mingine mipya ya Amani, walipoifunga Azam kwa mikwaju ya
penalti katika fainali iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar, kabla ya
kufanya hivyo kwenye michuano ya Super 8, juzi, ikiwa imeanzishwa kwa
mara ya kwanza |
No comments:
Post a Comment