Mlinzi wa Arsenal, Bacary Sagna, na ambaye pia ni mchezaji wa kimataifa
wa Ufaransa, ameelezea wasiwasi kuhusiana na mipango ya usajili ya
klabu.
Timu ya The Gunners imemruhusu Robin van Persie na
Alexander Song kuondoka msimu huu wa joto, na mwaka jana iliwaachia
wachezaji Cesc Fabregas, Samir Nasri na Gael Clichy kuondoka.
"Mwezi
Mei niliitizama timu ya Manchester City katika televisheni
wakishangilia ushindi wao. Nilimtizama Samir na Gael wakiliinua kombe.
Hilo linakufanya utamani kufanya vivyo hivyo."
"Nilitazamia Robin kuondoka," alisema Sagna, mwenye umri wa miaka 29, alipohojiwa na gazeti la Ufaransa, L'Equipe.
"Lakini nilishangazwa na kuondoka Alex. Ana umri wa miaka 24, na alikuwa na miaka mitatu iliyosalia katika mkataba wake.
"Unapowatizama kati ya wachezaji wawili bora zaidi uliokuwa nao msimu uliopita wakiondoka, basi unaanza kujiuliza maswali."
Mshambulizi
Van Persie alinunuliwa na Manchester United baada ya kuelezea kwamba
hana nia ya kutia saini mkataba mpya na timu ya Gunners, na Song
alielekea Barcelona.
"Mitaani, baadhi ya mashabiki huzungumza nami. Ninaelewa wamekasirika. Mimi ni kama wao, sielewi yote," aliongezea Sagna.
Nasri na Clichy walijiunga na Manchester City mwaka 2011, na kukisaidia klabu kupata ubingwa wa Premier msimu uliopita.
Sagna alijiunga na Arsenal kutoka klabu ya Auxerre mwezi Julai mwaka 2007, na ameichezea Arsenal mechi 205.
Hivi sasa amepumzishwa, kwani bado anaendelea kupona baada ya kuvunjwa mguu katika mechi dhidi ya Norwich mwezi Mei.
Mkataba
wake utakwisha mwisho wa msimu wa mwaka 2013-14, na alipoulizwa kama
kuna yeyote ambaye ameshauriana naye kuhusiana na mkataba mpya, alisema
"La, hakuna yeyote aliyezungumza nami."
|
No comments:
Post a Comment