Neymar na mwanae ambaye anamgharimu zaidi ya $15,000 kwa mwezi kumlea.
Miezi kadhaa iliyopita vyombo vya habari
vya Brazil vilikuwa vinapotosha na kusema kwamba Neymar anaingiza kiasi
cha $18 million kwa mwaka, jambo ambalo lilikuja kuonekana sio sahihi
pale alipoanza kufanya mazungumzo mapya juu ya mahitaji yake kwenye
mshahara mpya na klabu yake ya Santos. Kwa maana hiyo Neymar bado
hajaweza kuingiza fedha nyingi kiasi cha kuweza kununua matoi ya
kuchezea kwa matajiri kama boti za Yatch. "Kiukweli anatumia fedha
nyingi sana karibu na kile chote anachoingiza," anasema mtaalam wa mambo
ya fedha wa jarida la Forbes bwana Settimi huku akisisitiza lazima
klabu yake itakuwa inamsaidia kwa kumpa fedha nyingine nje ya mkataba
wake. "Inawezekana Santos wana mkono wao kwa
sababu ukiangalia matumizi yake ndani ya kipindi cha miaka miwili
iliyopita unaona kwamba ametumia zaidi ya kile alichoingiza - kuna
taarifa zinasema klabu yake inampa fedha nyingi hata nje ya mkataba ili
kumridhisha na kumfanya asahau kwenda barani ulaya."
Mhariri mkuu wa jarida la Forbes
Kurt Badenhausen anamfananisha Neymar na Mike Tyson: " neymar ndio
kwanza anakuwa na anatengeneza fedha nzuri sana. Kama ilivyokuwa kwa
Tyson ambaye nae alianza kutengeneza fedha akiwa na miaka 18 na miaka
kadhaa baadae alikuwa na utajiri wa $400 million - hivi ndivyo nahisi
Neymar akavyokuwa ikiwa itaacha kutumia vibaya fedha zake."
Mike Tyson akiwa kwenye kiwango cha
juu, pambano lake moja alikuwa akitia ndani kiasi cha $30 million.
Lakini wakati wa kipindi hicho, Tyson alinunua mahekalu, magari ya
kifahari, chui wa kufuga. Mwishoni mwa mwaka 2002, aliingia kwenye duka
la kuuza vito na kununua cheni ya dhahabu yenye thamani ya $174,000
huku ikiwa imenakishiwa na almasi kiasi. Miezi nane baadae Tyson
akatangaza kufulisika huku akiwa na madeni yanayofikia $23 million.
Watu wengine maarufu ni kama vile
star wa NBA Antoine Walker, ambaye alitengeneza zaidi ya $110 million
wakati akicheza bado, na Evander Holyfield, wote wamefilisika.
Mfano mwingine mzuri haupo mbali na
yeye. Nchini Brazil mwanasoka Romario, ambaye alikuwa mchezaji muhimu
sana kwa Brazil katika fainali za kombe la dunia 1994, alikamatwa mwaka
2009 kwa kesi ya kushindwa kutoa fedha ya malezi ya mtoto. Huku akiwa
na deni linalofikia $5 million.
Neymar anatakiwa kufuata mfano wa
gwiji wa soka wa nchi hiyo Ronaldo De Lima ambaye aliwekeza fedha zake
vizuri. Ronaldo sasa hivi anamiliki asilimia 45 za kampuni ya 9ine
Sports and Entertainment Agency, kampuni inayodili na masuala ya soka,
ambapo moja ya wateja wao ni Neymar.
Shukrani kwa 9ine inayofanya vizuri
sana kwenye biashara zake, Ronaldo de lima sasa ana thamani ya utajiri
unaofikia $250 million. Kwa maana hiyo Neymar itabidi afuate nyayo za
huyu jamaa ili aweze kuwa na mafanikio miaka kadhaa ijayo, na sio
kufuata nyayo za Romario na akina Tyson.
| |
No comments:
Post a Comment