Raisi wa shirikisho la soka Senegal
(FSF) Augustin Senghor amesema tukio la vurugu lilotokea siku ya
jumamosi ilikuwa hujuma iliyopangwa kuharibu soka la nchi hiyo na
kuliharibia sifa shirikisho hilo.
Boss wa FSF alisema ilitolewa oda ya
tiketi kutoka mtu binafsi na tiketi zikagawawiwa kwa wahuni kwa dhumuni
la kufanya vurugu katika mechi ya Senegal na Ivory Coast katika mechi ya
marudiano ya kufuzu kushiriki AFCON 2013, mechi ambayo kwa bahati mbaya
iliishia dakika ya 76 baada ya kuibuka kwa vurugu katika uwanja wa watu
60,000 uitwao Leopold Senghor jijini Dakar.
"Kuna mtu alitoa oda ya tiketi nyingi
na akazigawa kwa wahuni waliofanya vurugu kwenye mechi. Wanataka
kuharibu siafa ya ya soka la nchi yetu, ili waweze kutusema vibaya siku
za mbele kwa mashabiki na taifa zima kwa ujumla," alisema.
Mapema Jumatatu, winga wa Leeds United
El Hadji Diouf alisema wazi kwamba walizizuia tiketi 1,000 alizotoa oda
kwa ajili ya kugawa kwa mashabiki, kutokana na shirikisho kuhisi kwamba
mchezaji huyo alikuwa amewakusanya wahuni ili wakafanye vurugu uwanjani
na kuitibua mechi.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kilicho
karibu na shirikisho la FSF, Diouf alikuwa ndio mtu binafsi peke
aliyenunua tikieti nyingi kwa ajili ya mchezo huo.
Japokuwa mchezaji huyo amesema hahusiki
na chochote kuhusu vurugu za usiku wa Jumamosi, huku akiisisitiza
serikali kuwaondoa viongozi wote wa shirikisho na kuliunda upya. |
No comments:
Post a Comment