Kupitia vyombo mbalimbali vya
habari vinavyotoa michapo ya michezo kila siku nchini U.K vimeipa stori
ya Ashley kichwa cha habari “Chelsea wanaweza kumuuza Cole January
mwakani”
PSG ya Ufaransa iliyopanga
kumnunua mchezaji huyu staa wa Chelsea, unaambiwa zipo club nyingine
kubwa kwenye list ambazo ni Real Madrid, Man U na Man City ambazo ziko
tayari kutoa poundi laki moja na nusu kila wiki na mkataba wa miaka
mitatu unaoaminika kuwa na thamani ya pound milioni 23.
Baada ya Ashley Cole kushindwa
kufikia makubaliano ya mkataba mpya na Chelsea, club tajiri ulaya
ikiwemo PSG zimetangaza nia ya kumsajili staa huyu mwenye umri wa miaka
31.
Kama Ashley Cole na Lampard
wataondoka Chelsea, wataalamu wa mambo wanasema timu hii iliyochukua
ubingwa wa Ulaya itakua imesambaratika japo inasemekana kwamba mmiliki
wake amepanga kuhakikisha hivyo vichwa haviondoki, tofauti na tetesi
zilizo kwenye vyombo vya habari. |
No comments:
Post a Comment