Mchezaji kiungo wa timu ya Afrika Kusini,Thulani
Serero huenda akakosa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za mwaka
2013 zitakazofanyika nchini Afrika Kusini kutokana na maumivu ya nyonga
aliyopata mwezi uliopita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye
anachezea timu ya Ajax nchini Uholanzi, aliumia wakati wa mechi dhidi ya
timu ya ADO Den Haag iliyofanyika tarehe 23 Septemba na hataweza
kucheza hadi mwezi Januari mwaka kesho.
" Hatutarajii kupona haraka na
kushiriki katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika akiichezea timu
yake ya taifa ya Bafana Bafana," umesema uongozi wa Ajax.
"Hata kama atapona haraka, klabu pamoja na mcezaji mwenyewe, inabidi tuwe makini kuhusu hali yake."
Klabu ya Ajax imeongeza kuwa: "Thulani alikumbwa
na majeraha madogo madogo msimu uliopita na sasa alikuwa mchezaji wa
mara kwa mara kwa timu ya Ajax, kwa hiyo tatizo hili ni gumu kwake."
Kukosekana kwa Serero katika timu ya Bafana
Bafana ni pigo kubwa kwa Afrika Kusini, hususan baada ya nahodha wa timu
hiyo kutangaza hivi karibuni kwamba anastaafu soka la kimataifa.
Ina maana kwamba litakuwa pengo kubwa kuwakosa
wachezaji viungo wawili wa kutegemewa na kutaathiri nafasi ya timu ya
Bafana Bafana kushinda katika ardhi yake. |
No comments:
Post a Comment