Wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani
watapokea kiasi cha €20,000 kwa kila mechi ya kufuzu kombe la dunia
watakayocheza na ikiwa watafanikiwa kufika nchini Brazil 2014, chama cha
soka cha hiyo DFB kimethibitisha.
Kila mchezaji atapata kiasi hicho chote
cha fedha kwa kila mechi ya kufuzu, lakini watapokea kiasi hicho mara
watakapoweza kufuzu kwenda kwenye michuano ya hiyo ya dunia
itakayofanyika nchini Brazil 2014.
"Nina furaha na uharaka na kutokuwepo
kwa matatizo katika makubaliano haya. Hii inaonyesha uaminifu uliopo
kati ya shirikisho na wachezaji wa timu ya wakubwa ya soka ya
Ujerumani," alisema Raisi wa shirikisho hilo Mr.Wolfgang Niersbach.
Ujerumani tayari wameshashinda mechi zao
mbili za kundi C na mpaka sasa wanapewa nafasi kubwa ya kuwa viongozi
wa kundi hilo kwa kuongeza pointi 6 nyingine watakapocheza na Irealnd
na Sweden Ijuma na Jumanne ijayo.
|
No comments:
Post a Comment