Utafiti uliofanywa kuhusiana na uamuzi wa marefa uwanjani
katika mechi za ligi kuu ya Premier, unaonyesha kwamba waamuzi kwa jumla huenda
wakawachulia hatua wachezaji wa kigeni kwa asilimia 15, kinyume na vile
wanavyoweza kuwaadhibu wachezaji wa Uingereza.
Maelezo ya utafiti huu, yaliyochapishwa pia katika mtandao wa kijamii wa
Tweeter, unaonyesha waamuzi ni wepesi wa kuwaadhibu wachezaji wachezaji walio
wachache nchini Uingereza umefanywa na vyuo vikuu vya Birmingham, Cambridge na
Oxford, na ulitumia takwimu zilizokusanya na OPTA Sportsdata, katika misimu ya
ligi mwaka 2006-07 na 2007-08.
Utafiti huo ulikagua mechi 760 kwa jumla.
Utafiti ulikusanya ushahidi kutoka kwa hatua zote za mchezo (kwa mfano
katika kuangalia migongeo na chenga), katika mechi zote, na vile vile maelezo
kuwahusu wachezaji, kwa mfano nambari wanayocheza uwanjani, umri wao, urefu na
ukubwa wa mchezo (kwa mfano, mechi kuu ya watani wa jadi mtaani).
Kwa
kukusanya takwimu mbalimbali, watafiti waliepuka dhana kwamba kuonywa mara kwa
mara wachezaji fulani kulimaanisha mchezo wao ni hatari.
Kinyume na
hayo, watafiti wanaamini kwamba kwa njia moja, uchunguzi wao ulithibitisha kuna
hali ya waamuzi kubagua pasipo kukusudia.
Hii ni hali ya jamii moja
katika jamii kuwa na mawazo kwamba kundi fulani huwa na tabia za
kutoridhisha.
Dk James Read wa chuo kikuu cha Birmingham anaeleza:
"Matokeo ya utafiti yanaonyesha dhahiri kwamba waamuzi wamo katika hali ya
kuandikisha makosa ya wachezaji wa kigeni moja kwa moja, kwa kuwa ni wa kutoka
kwa jamii za waliowachache nchini Uingereza.
"Kwa upeo mkubwa
tuliangalia masuala mengi kama anavyocheza mchezaji, umri na nafasi yake
uwanjani, na katika kila mechi. Kwa hiyo tuna imani kwamba uamuzi unaoafikiwa na
waamuzi sio kutokana na hali ya mchezo, lakini ni kwa kuangalia masuala
mengine."
Mchezaji wa Manchester City, Sergio Aguero, kutoka Argentina, hivi majuzi
alilalamika kwamba wachezaji wa kigeni huonea na waamuzi katika mechi za ligi
kuu ya Premier, wakijilinganisha na wachezaji wenzao Waingereza.
|
No comments:
Post a Comment