Klabu ya Newcastle siku ya Jumanne ilitangaza kwamba
itapata pauni milioni 24 kutoka kwa wadhamini wapya, kupitia kuvaa
mavazi yao, kampuni inayotoa mikopo ya Wonga, lakini Baraza la Waislamu
nchini Uingereza, Muslim Council of Britain, limesema ikiwa wachezaji wa Kiislamu watavaa mavazi hayo, hilo litakuwa ni kinyume cha sharia kulingana na dini.
Baadhi ya watu wamelalamika kuhusiana na klabu
kutia saini mkataba wa muda mfupi na kampuni hiyo ya Wonga, na sasa
Baraza la Waislamu nchini Uingereza, MSB, limeingilia kati suala hilo.
Mkataba huo na Wonga ni wa miaka minne.
Wachezaji wanne ambao ni waislamu walishiriki
katika mechi dhidi ya wageni Manchester United siku ya Jumapili, mechi
ya ligi kuu ya Premier; Demba Ba, Papiss Cisse, Cheick Tiote na Hatem
Ben Arfa – na wote wamehimizwa kuelezea msimamo wao.
Sheikh Ibrahim Mogra, naibu wa katibu mkuu wa
MCB amesema: "Kuna masuala mawili katika hili. Kuna kanuni za dini
katika suala hili, na vile vile kuna uamuzi wa mtu binafsi, na
kuzingatia au kutozingatia kanuni hiyo.
"Nia ni kuwalinda wale ambao ni dhaifu na huenda wakakandamizwa na kutumiwa na wenye mamlaka na matajiri.
"Wakati wanapotoa mikopo na kutoza kiasi kikubwa
cha riba, hilo linamaanisha maskini hunufaika kwa muda mfupi kutokana
na mkopo, lakini matatizo ya baadaye ni ya muda mrefu wanaposhindwa
kulipa mikopo, kwa kuwa huwa ni vigumu kuendelea kuwaza kulipa riba
hiyo."
Aliongezea: "Mfumo wa Kiislamu huepuka kuzingatia kunfuaika kwa kutoza riba."
Klabu kimekuwa kikijaribu kukwepa shinikizo
hizo, na baada ya mkataba huo, kimetangaza kwamba kitabadilisha jina la
uwanja wake kutoka Sports Direct Arena, na kulitumia jina la zamani la
St James' Park.
Hata hivyo wengi wameendelea kukilaumu klabu kwa
kukubali kutia saini mkataba na kampuni ya Wonga, na wamekuwa
wakielezea namna wameudhika, hasa kupitia mitandao mbalimbali ya jamii. |
No comments:
Post a Comment