Louganis alipoumizwa na ubao akiogelea mwaka 1988 mjini Seoul
Nepal itakuwa ni nchi ya kwanza Asia ya Kusini kuwa
mwenyeji wa mashindano ya wanamichezo wanaoshiriki katika mapenzi ya
jinsia moja, wale wanaovutiwa na wanawake na vile vile wanaume, na pia
wale ambao wamebadilisha jinsia moja hadi nyingine.
Mashindano hayo, yanayojulikana kama lesbians,
gays, bisexuals, transgendered and intersexes, kwa kifupi LGBTI, ni
mashindano ya siku tatu ambayo yanaanza Ijumaa.
Zaidi ya wanamichezo 350 watakuwa ni kutoka Nepal, na wengine 150 watakuwa ni kutoka mataifa 17 kote ulimwenguni.
Kati
ya wanariadha wanaofahamika ni pamoja na mwanamichezo maarufu wa
Olimpiki, Gregory Efthimios Louganis, ambaye anajulikana zaidi miongoni
mwa mashabiki wa michezo kama Greg Louganis.
Mwogeleaji huyo wa
Marekani, ambaye alishinda medali mbili mbili katika mashindano ya
Olimpiki miaka ya 1984 na 1988, amekubali atafika katika mashindano hayo
ya Kathmandu kama mgeni mheshimiwa.
Louganis anafahamika kwa
kuwasaidia wanamichezo kuimarisha vipawa vyao kote ulimwenguni, na
kuwepo kwake katika mashindano hayo ni jambo ambalo linasemekana
litayapa uzito.
Mashindano hayo pia yatawapa nafasi ya
wanaoshiriki katika mashindano ya LGBTI kuendelea kuzitetea haki zao,
hasa nchini Nepal, walielezea waandalizi kutoka shirika la Blue Diamond
Society.
Kati ya yale yanayokumbukwa kumhusu mwanariadha
Louganis ni wakati alipoumizwa na ubao alipokuwa anaruka majini katika
mashindano ya Olimpiki mjini Seoul, mwaka 1988.
Licha ya kuumia na kushonwa kichwa, alifanikiwa kushiriki katika mashindano, na akawa mshindi.
Baadaye iligunduliwa kwamba miezi sita kabla ya mashindano ya Olimpiki, kumbe alikuwa akiishi kwa viini vya HIV.
Louganis
alifichua mwaka 1994 kwamba alikuwa akishiriki katika mapenzi ya jinsia
moja, na aliandika kitabu, 'Breaking the Surface', akielezea baadhi ya
masaibu yaliyompata mapema maishani, ikiwa ni pamoja na kukandamizwa,
kutomaswa na akiishi katika hali ya kusononeka mno maishani. | |
No comments:
Post a Comment