UONGOZI wa Simba
SC unapenda kuzungumza yafuatayo
kuhusiana na matukio ya karibuni kuhusiana na klabu ya Simba.
- Uongozi
umesononeshwa na matokeo ya siku za karibuni ya timu ya Simba hususani
yale ya kufungwa mabao 2-0 na Mtibwa Sugar ya Morogoro. Kutokana na hali
hiyo, Kamati ya Utendaji ya Simba imeliagiza benchi la ufundi la Simba
kutoa ripoti kuhusiana na mwenendo wa timu katika mechi za karibuni.
Ikumbukwe kwamba Simba ilianza
ligi kwa vishindo na hadi kufikia mechi ya 12, ilikuwa ikiongoza ligi na
ilikuwa timu pekee ambayo haikuwa imepoteza mechi.
Mara baada ya ripoti ya benchi la
ufundi kukamilika, Kamati ya Utendaji ya Simba itakutana na kutoa maamuzi
kuhusiana na yaliyomo kwenye ripoti. Kutokana na hali hiyo, uongozi unaomba
wapenzi na wanachama wake kuwa watulivu katika kipindi hiki ambapo uongozi na
benchi la ufundi linatafuta suluhisho la kudumu kuwezesha timu kuendelea
kushinda.
Hata hivyo, uongozi wa Simba
unasisitiza kwamba hakuna kiongozi yeyote wa Simba –kuanzia wa juu zaidi hadi
wa chini zaidi, ambaye amejiuzulu au kuachia ngazi ndani ya klabu.
Ifahamike kwamba uongozi huu
ulipewa dhamana na wanachama miaka minne iliyopita ya kuiongoza klabu kisasa na
kuipa maendeleo endelevu kwa kipindi hicho.
Chini ya uongozi huu, Simba
ilikuwa mshindi wa pili misimu miwili iliyopita (ikiwa pointi sawa na mabingwa
ila ikizidiwa kwa pointi, ilikuwa mabingwa msimu uliopita, iliingia hatua ya 16
bora michuano ya CAF, imesajili wachezaji msimu huu kwa fedha zake yenyewe
(miradi mbalimbali) na inaendesha timu tatu za vijana.
Bado kuna kazi za kufanya na
uongozi unatambua hilo.
Ndiyo maana uongozi hauamini kwamba maneno mabaya yanayosambazwa dhidi ya
viongozi yanatoka kwa wanachama wake. Kazi nzuri ya uongozi huu inaonekana na
iko dhahiri.
Uongozi wa Simba unaomba wapenzi
na wanachama wake kuwa wamoja katika kipindi hiki ili kuwezesha ushindi
kupatikana dhidi ya Toto African ya Mwanza Jumamosi ijayo.
2. Kuhusu mchezaji Juma Kaseja
|
No comments:
Post a Comment