Baada ya leo asubuhi kutoa maoni kwa
klabu ya AZAM ya kumuondoa kikosini nahodha Aggrey Morris kama kweli
alihusika na tuhuma za rushwa,hatimae hivi punde nimepata taarifa kutoka
kwenye chanzo cha kuaminika beki huyo na nahodha wa timu hiyo
ameondolewa kwenye kikosi na kocha Stewart Hall.
Tayari Morris alikuwa mjini Tanga pamoja
na kikosi cha Azam kinachojiandaa na mchezo dhidi ya JKT MGAMBO hapo
kesho amerejeshwa jijini Dar Es Salaam,kocha Stewart Hall amemuondoa
nahodha huyo kikosini baada ya kuonyeshwa vielelezo vya
wachezaji waliohusishwa na tuhuma za kuchukua rushwa ili kuifungisha
Azam, kitendo ambacho kimewaudhi sana wachezaji wa Azam.
I SALUTE YOU AZAM KTK HILI!Nawaomba
kamwe msirudi nyuma it's time now kwa ajili ya kutokomeza rushwa
michezoni hasa mchezo wa soka. |
No comments:
Post a Comment