Mjumbe Mwarami Kobe Ally ( kushoto ),mwenyekiti,Juma Simba (kati ) na Katibu wa kamati bwana Peter Hella (kulia ) .
Mgombea asiyeudhuria usaili apitishwa kugombea
WAKATI majina ya
wagombea katika uchaguzi mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) yakiwekwa hadharani, majina ya wagombea Said Tully,Ally Mayay na
Philemon Ntahilaja yamekatwa huku Isaac Mazwile akipitishwa bila hata ya
kuwepo katika usaili.
Awali
Tully ambaye ni wakala anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la
Kimataifa (Fifa) aliwekewa pingamizi la kutokuwahi kufanya kazi katika
klabu ya Ashanti United ya Ilala na hata alipowasilisha barua ya
kuchaguliwa katika moja ya kamati za timu hizo, alitupwa nje.
Mbali
ya Mazwile kupitishwa kuwania nafasi ya mwakilishi wa mkutano mkuu wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na makamu mwenyekiti, mtu mwingine
aliyepitishwa ni Muhsin Balbhou anayewania nafasi ya mwakilishi wa
mkutano mkuu huku akiwa amewekewa pingamizi.
Uteuzi wa Mwarami Ally Kobe kwa mara ya pili katika kamati ya uchaguzi
Kwa mujibu wa
mmoja wa wagombea wa nafasi ya uwakilishi wa mkutano mkuu, Shaffih
Dauda, mjumbe wa kamati hiyo Ally Kobe, hakustahili kuchaguliwa tena
kuwamo ndani ya kamati hiyo kwani alishiriki madudu ya awali
yaliyoifanya kamati iliyokuwa chini ya Mwenyekiti, Muhidin Ndolanga
kuvunjwa na TFF.
Hivi
karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Deo Lyato alivunja
kamati ya uchaguzi ya DRFA iliyokuwa chini ya Ndolanga kutokana kukiuka
kanuni mbalimbali za uchaguzi huku kubwa likiwa kutia kasoro fomu za
wagombea kadhaa.
Kobe
anadaiwa kuhusika kwa kiasi kikubwa katika madudu hayo, lakini
Mwenyekiti wa DRFA anayemaliza muda wake, Said Bakhressa ambaye
ameenguliwa na kamati ya Lyato kutetea nafasi yake, alihakikisha Kobe
anabaki katika kamati ili tu kuhakikisha mtandao wake wa viongozi
unapitishwa kuwania uongozi DRFA.
Hivyo,
Kobe aliachwa ili kuwalinda baadhi ya wagombea wanaodaiwa kuwa ama
wafuasi au kupandikizwa na Bakhressa katika mchakato wa usaili hata
mapingamizi wanayowekewa.
Ili
haki itendeke, ilitakiwa Kobe asiwepo tena katika kamati mpya ili
kufanya mambo yaendelee katika mstari mnyoofu kwani lengo la Lyato
lilikuwa kuhakikisha haki inapatikana katika mchakato wa uchaguzi huo.
Hii ina maana si Ndolanga peke yake aliyekuwa na matatizo katika kamati
hiyo.
Inaweza
hata mambo yaliyotokea wakati mwenyekiti akiwa Ndolanga, yalisababishwa
na wajumbe kama kina Kobe. Kwa hali hii, hakuna jipya lililofanywa na
Lyato, kwani madudu yameendelea.
Miongoni
mwa mambo yaliyofanywa na kamati ya sasa ya uchaguzi ya DRFA iliyo
chini ya Mwenyekiti, Juma Simba ‘Gaddafi’ ni kupitisha majina ya Mazwile
na Balhabou huku wakiwa wamewekewa mapingamizi na wagombea wenzao.
Gaddafi kutokuwepo katika kamati kwaruhusu madudu
Katika
kikao cha kupitia mapingamizi yaliyowekwa kwa baadhi ya wagombea wa
uchaguzi wa DRFA, mwenyekiti, Juma Simba hakuwepo kutokana na udhuru
aliotoa ili kuhudhuria mambo ya siasa katika Chama cha Mapinduzi (CCM) ambako ana majukumu.
Kwa
kutumia mwanya huo, wajumbe Said Rubeya na Kobe walitumia kila njia
kuhakikisha wanawabeba baadhi ya wagombea ambao ndani yake wapo Mazwile
na Balhabou.
Hata
katibu wa kamati, Peter Hella alizidiwa nguvu na Rubeya na Kobe katika
kuhakikisha haki inapatikana jambo lililomfanya achukue uamuzi wa
kujiuzulu kwa kutokubaliana na kilichokuwa kikifanywa na wajumbe hao.
Kuona
hivyo, mwenyekiti Gaddafi alipopewa taarifa hizo na Hella, alimsihi
katibu huyo asijiuzulu kwa ahadi ya kuzidi kuuchafua uchaguzi huo. Hella
bado yupo mguu ndani mguu nje kuhusu nafasi yake kwenye kamati hiyo.
Pingamizi la Mazwile lilivyozimwa.
Mgombea Mazwile
aliwekewa pingamizi na Shaffih Dauda linalohusu kitendo chake cha
kutokuwa mwadilifu katika kazi zake akiwa mtendaji wa Chama cha Soka
Kinondoni (KIFA) kwa kumruhusu mtu asiye kiongozi kusaini kazi za chama
hicho.
Inadaiwa
kuwa, Mazwile akiwa mtendaji wa KIFA alitakiwa kusaini fomu za wagombea
mbalimbali waliokuwa wakitakiwa kuhalalishwa kugombea katika vyama
mbalimbali vya soka ikiwemo DRFA ili kuthibitishwa uhalali wao.
Akijua ni kinyume na taratibu, Mazwile akiwa safarini mkoani Dodoma aliruhusu mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Seif Ally Mailo 'Saddam' alisaini fomu na karatasi nyingine zilizopita KIFA kwa niaba yake, ikimbukwe Saddam hana madaraka yoyote KIFA.
Katika
pingamizi hilo, vithibitisho vilitolewa ikiwemo karatasi zilizosainiwa
na Saddam kwa niaba ya Mazwile lakini kamati ya uchaguzi kupitia wajumbe
wakina Rubeya na Kobe, walitupilia mbali pingamizi hilo. Hata katibu
ambaye ni Hella alipowataka wajumbe wenzake kutazama kwa mara ya pili
pingamizi hilo, alipingwa vikali. Hatimaye, pingamizi la Mazwile
lilitupwa mbali.
Pingamizi la Balhabou nalo utata mtupu
Katika pingamizi
lake kwa Balbhou, Shaffih Dauda alikuwa alipinga mgombea huyo kuwa na
elimu ya kidato cha nne inayotakiwa kwa kila mgombea wa uongozi wa DRFA
kwa sasa.
Kamati
ilitoa jibu la kuhakika vyeti vya Balbhou lakini ikimruhusu kuendelea
na mchakato wa uchaguzi jabo ambalo ni kinyume na taratibu za uchaguzi
huo. Hivyo pingamizi hilo nalo lilitupwa na kamati huku nguvu kubwa
ikitoka kwa Rubeya na Kobe.
Kwa
kawaida taasisi inayotakiwa kuthibitisha elimu ya kidato cha nne nchini
ni Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) na mchakato huo unaweza kuchukua
siku saba hadi 14 tu.
Mazwile hakuhudhuria usaili lakini kamati yampitisha
Madudu mengine
yaliyofanywa na kamati ya uchaguzi ya DRFA ni kupitisha jina la Mazwile
kuwania nafasi ya uwakilishi wa mkutano mkuu na makamu mwenyekiti bila
ya kuhudhuria usaili wa wagombea wote uliofanyika katika ukumbi wa
Uwanja wa Uhuru.
Mmoja
wa wagombea wa uchaguzi wa DRFA, Shaffih Dauda alikuwepo ukumbini tangu
mwanzo hadi mwisho na hakumuona Mazwile kuhudhuria usaili huo, lakini
jambo la ajabu jina la mgombea huyo limeorodheshwa katika majina ya
wagombea waliopitishwa kuwania uongozi DRFA.
Hayo
ni baadhi tu madudu yaliyofanywa na kamati ya uchaguzi ya DRFA ambayo
inasimamia uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
from http://www.shaffihdauda.com/
|
No comments:
Post a Comment