Zoezi la klabu bingwa ya Tanzania bara
Simba kupata mbadala wa beki wake aliyetimkia Yanga, Kelvin Yondani
linaendelea, baada ya Lino Musombo kutemwa na kusajiliwa kwa Keita na
Ocheing ambao wameonekana kuhangaika kuziba pengo la Yondani, sasa klabu
hiyo ya Simba inasemekana wapo katika harakati za kumrudisha moja wa
mabeki wao bora katika kipindi cha miaka 10 iliyopita mganda Joseph
Owino.
Simba ambao walianza ligi vizuri na
kuongoza ligi kwa muda mrefu kabla ya kupoteza muelekeo mwishoni mwa mwa
raundi ya kwanza ya msimu wa VPL. Sasa katika kujaribu kuimarisha safu
ya ulinzi ya timu hiyo ambayo imeonekana kuyumba sana msimu huu, uongozi
wa Simba umeona bora ufanye mpango wa kumrudisha kundini Owino ambaye
amesajiliwa Azam lakini amekuwa akikosa namba ya kudumu baada ya kurudi
kutoka kwenye majeruhi yaliyomuweka nje kwa muda mrefu.
Taarifa ambazo hazijathibitishwa ni kwamba Simba tayari wapo kwenye mazungumzo na Azam ili kuweza kuona uwezekano wa kumsaini Owino.
Owino ambaye aliondoka Simba baada ya
kupata majeraha ya goti ambayo yalimuweka nje kwa muda mrefu, na Azam
wakamsajili akiwa mgonjwa wakamtibu lakini baada ya kupona amekuwa na
urafiki mzuri na benchi la Chamazi. |
No comments:
Post a Comment