Wadhamini wa Timu ya Taifa (Taifa
Stars), Kilimanjaro Premium lager, wamesema wanarishishwa na kiwango cha
timu hiyo kwa sasa hku wakiomba TFF iandae mechi nyingi za Staridi za
kirafiki hapa nyumbani. Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Bia ya
Kilimanajro Premium Lager, George Kavishe siku moja baada ya Stars
kuicharaza Cameroon bao 1-0 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa katika
Uwanja wa Taimu hiiifa Jijini Dar es Salaam. “Kwa kweli tunafurahishwa na mafanikio
ya timu hii tangu tuchukue udhamini mwezi Mei mwaka jana….tumeiangalia
ikicheza ndani na nje na kwa kweli kikosi ni kizuri kwani kimewaletea
watanzania ushindi,” alisema.
Aliwapongeza watanzania kwa kujitokeza
kwa wingi kuishangilia timu yao kama kauli mbiu ya KIlimanajro Premium
Lager inavyosema…”Sherekea kilicho chetu.
“Hawa walikuwa wanajulikana kama Simba wa Afrika lakini wameondoka wakiwa wamenyong’onyea baada ya kufungwa 1-0,” alisema.
Bw Kavishe alisema ushindi huu wa Stars
umewapa nafasi nzuri ya kuendelea kuidhamini Taifa Stars ili kuwapa
watanzania nafasi ya kusherekea kilicho chao kwa kupitia burudani ya
mpira.
| |
No comments:
Post a Comment