Mabingwa wa ligi ya Ujerumani
Bayern Munich wamekamilisha wiki nzuri kwao kwa kuandika historia mpya
ya kuwa bingwa mwenye idadi kubwa ya pointi kuliko wote kwenye
Bundesliga.
Bayern imefikisha jumla ya
pointi 83 baada ya kuifunga Freiburg 1-0 kwenye mchezo wa ligi uliopigwa
mapema april 27 2013 ambapo ni goli lililoipa Bayern ushindi lilifungwa
na kiungo Xherdan Shaqiri ambapo limeifanya timu hiyo kufikisha pointi
84 huku ligi ikiwa imesaliwa na michezo mitatu kabla ya kumalizika.
Bayern wanamaliza wiki ambayo
ilianza kwa taarifa ya kusajiliwa kwa kiungo Mario Gotze kabla ya
ushindi wa 4-0 kwenye mchezo wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa dhidi
ya Fc Barcelona ambao uliifanya Bayern kuweka mguu mmoja kwenye fainali
ya michuano hiyo.
Bayern wamevunja rekodi iliyowekwa na mabingwa wa msimu uliopita Borrusia Dortmund ya pointi 83 . |
No comments:
Post a Comment