Wachezaji wote wa mabingwa
wapya wa ligi kuu ya England watapata medali za ubingwa wa ligi kuu ya
England baada ya chama cha soka che England na ligi kuu kulegeza
masharti yaliyokuwa yanabana idadi ya wachezaji wanaoweza kupewa medali
pale timu inapotwaa ubingwa.
Katika misimu ya miaka ya nyuma
wachezaji waliokuwa wanaweza kupewa medali baada ya timu kuwa bingwa ni
wale waliocheza idadi ya mechi 10 na zaidi huku magolikipa pekee wakiwa
na nafasi ya upendeleo, zaidi ya hapo kama idadi ya medali ni ndogo
timu ilikuwa inatakiwa kutuma maombi maalum ambayo yalihitaji kuridhiwa
na FA kuhusu medali za ziada.
Hata hivyo kwa sheria mpya ya
ligi kuu ya England, wachezaji wanaoweza kuvaa medali ni wale waliocheza
mechi tano na zaidi huku timu inayotwaa ubingwa ikipewa medali 40 na
kutakiwa kutuma maombi kwa wale wanaoweza kuwa wamekosa medali hizo.
Kwa sheria za zamani wachezaji
Darren Fletcher, Alexander Buttner na Nick Powell wasingeweza kupewa
medali huku kipa Anders Lindergaard akipata kwa sababu sheria hiyo
ilikuwa haiwahusu makipa, hata hivyo kwa sasa wachezaji hawa watapata
medali kama kawaida huku kukiwa na nyongeza ya kutosha kuwapa wachezaji
wengine wa kikosi cha kwanza ambao hawapati nafasi za kucheza kama Ben
Amos, Jesse Lingard na Marnick Vermijl na mchezaji Adnani Januzaj ambaye
anacheza kwenye kikosi cha U-18 ambaye amepewa jezi namba 44 huku kocha
Sir Alex Fergusson akiahidi kumpa nafasi kwenye mechi zilizobaki.
Fergie ameipa dole sheria hiyo
akisema kuwa iko ‘fair’ kwa kuwa kila mchezaji hata kama amecheza mechi
tatu kama kina Powell, Fletcher na Buttner anahesabika kuwa ametoa
mchango unaostahili medali.
|
No comments:
Post a Comment