Ilikuwa April 27 miaka 23
iliyopita wakati ndege iliyokuwa imebeba wachezaji 18 wa kikosi cha timu
ya taifa ya Zambia Chipolopolo, watu wanne wa benchi la ufundi akiwepo
kocha mkuu wa timu hiyo Godfrey Ucar Chitalu na wasaidizi wake watatu,
viongozi watatu wa chama cha soka cha Zambia ilipopata ajali mbaya
kwenye pwani ya Gabon na kuua watu wote 30.
Ndege hiyo aina ya DHC-5D
Buffalo ikiwa na namba za usajili (AF-319) ilianguka na kuzama kwenye
bahari ya Atlantic karibu kabisa na pwani ya mji mkuu wa Gabon
Libreville baada ya matatizo ya kiufundi ambapo kwa mujibu wa uchunguzi
uliofanywa na jeshi la Gabon, ndege hiyo ilipata hitilafu
iliyosababisha moto kwenye moja ya Injini zake hali iliyomlazimu rubani
Kanali Fenton Mhone kuizima injini hiyo, hata hivyo Rubani alikosea na
kuzima injini nyingine iliyokuwa nzima hali iliyofanya ndege hiyo
kushindwa kwenda vizuri na hatimaye kuanguka baharini.
Zambia ilikuwa njiani kuelekea
Senegal ilikokuwa inaenda kucheza na timu ya taifa hilo katika michezo
ya hatua za mwisho ya kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 1994 huko
Marekani.
Moja ya watu waliosalimika
kwenye ajali hiyo alikuwa nyota wa enzi hizo wa timu ya taifaya Zambia
Kalusha Bwalya ambaye hii leo ni Rais wa chama cha soka cha Zambia FAZ
ambaye alichelewa safari hiyo ambapo alikuwa anatokea nchini Uholamzi
alikokuwa anacheza soka la kulipwa .
Ajali hii ndio ajali mbaya
kuliko zote kwneye historia ya soka la Zambia na iliilazimu nchi hiyo
kuunda timu mpya kwa haraka ambayo iliongozwa na Kalusha Bwalya.
Cha kushangaza ni kwamba timu
mpya iliyoundwa kwa haraka haraka iliweza kufuzu kucheza kombe la
mataifaya Afrika mwaka uliofuatia ambapo ilifika fainali ilikofungwa na
Nigeria 2-1.
Hadi leo kikosi hicho ambacho
kilikuwa na wachezaji maarufu kama Kipa Efford Chabala , beki Eston
Mulenga ,kiungo Moses Chikwalakwala na mshambuliaji Patrick ‘The Bomber
Banda kinaaminika kuwa kikosi bora kilichowahi kutokea kwenye soka la
Zambia na wengi walitarajia kukiona kiiwakilisha Afrika kwenye fainali
za kombe la dunia Maka 1994.
Kocha wa timu hiyo Godfrey Ucar
Chitalu alipata umaarufu mkubwa enzi zake akiwa mshambuliaji wa klabu
ya Kabwe Warriors ambapo aliwahi kuweka rekodi a kufunga mabao 117
kwenye msimu wa mwaka 1972 rekodi ambayo FIFA imegoma kuitambua . Rekodi
hiyo ilitajwa sana. |
No comments:
Post a Comment