Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez ameomba radhi kutokana na
kitendo chake cha kumng'ata mkononi beki wa Chelsea Branislav Ivanovic
wakati timu hizo mbili zilipocheza jumapili jioni kwenye mchezo wa ligi
kuu soka nchini Uingereza.
Suarez,amesema binafsi anasikitishwa na kitendo
alichokifanya na amempigia simu Ivanovic na kumuomba radhi yeye mwenyewe
kwani anajutia kitendo alichomfanyia,na kushuruku kwa kuwa Ivanovic
amemsamehe.
Kitendo
hicho kilitokea katika kipindi cha pili cha mechi baina ya Liverpool na
Chelsea,Mechi iliyoishia kwa sare ya 2-2 huku Suarez akifunga bao la
dakika za mwisho la kuisawazishia Liverpool. Ivanovic alimuonyesha
mwamuzi Kevin Friend sehemu aliyong'atwa na Suarez lakini mwamuzi
alionekana kutotilia maanani kwa kuwa hakukiona kitendo hicho.
Wachambuzi wa masuala ya kandanda nchini
Uingereza wamekitaja kitendo hicho cha Suarez kama tukio lisilokubalika
katika mchezo wa soka,huku wakisema huenda akakabiliwa na adhabu kali
kutoka chama cha soka nchini Uingereza FA.
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema
ameangalia video ya tukio hilo mara baada ya mchezo na amesikitishwa na
kitendo hicho na kumueleza Suarez kuwa kitendo hicho hakikubaliki
michezoni,huku akisisitza kuwa hakuna mchezaji ambaye ni mkubwa zaidi ya
klabu hiyo. Naye Mkurugenzi wa klabu hiyo ya Liverpool Ian Ayre amesema
kitendo alichokifanya Suarez hakistahili kufanywa na mchezaji wa klabu
hiyo.Liverpool imesema itatoa adhabu stahili kwa kitendo hicho wakati
wakisubiri adhabu yoyote kutoka chama cha soka cha Uingereza FA.
Suarez sio wa kwanza kufanya kitendo cha
kumng'ata mchezaji uwanjani kwenye ligi kuu ya Uingereza,kwani mwaka
2006, mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Jermain Defoe alimng'ata kiungo
wa West Ham wa wakati huo Javier Mascherano katika mchezo wa ligi kuu
kwenye uwanja wa White Hart Lane.
Defoe alifanya kitendo hicho baada ya kuchukizwa
na rafu aliyochezewa na Mascherano ambapo mwamuzi Steve Bennett
aliwazawadia kadi za manjano wote wawili na baadaye chama cha soka cha
Uingereza FA kilisema hakitoa adhabu yoyote kwa kuwa mwamuzi alikiona
kitendo hicho na kuwaadhibu uwanjani. |
No comments:
Post a Comment