WINGA Shamte Ally ni kama amekata tamaa
kurudi tena Yanga kwa mara nyingine na sasa amepania kujikita kwenye
shughuli zake binafsi. Nyota wanne wa Yanga, Juma Seif
'Kijiko', Idrissa Rashid 'Messi', Shamte Ally 'B52' na beki Ibrahim Job
wametolewa kwa mkopo na timu hiyo kwenda kuinusuru African Lyon kushuka
daraja. Shamte alisema jijini Dar es Salaam kuwa mkataba wake
unamalizika Juni, mwaka huu, lakini hana tena matarajio iwapo klabu hiyo
itafikiria kumrejesha kwa mara nyingine.
"Mkataba wangu na Yanga unamalizika
mwezi Juni, mwaka huu. Lakini kwa hali inavyo kwa sasa siamini kama
watanirudisha tena. Kwa sasa nimeamua kupumzika kwanza nifanye mambo
yangu mengine." alisema Shamte ambaye alijiunga na Yanga akitokea Kagera Sugar ya Bukoba.
Ukweli ni kwamba, ujio wa Mrisho Ngassa
kwa mara nyingine kwenye kikosi cha Yanga na uwepo wa kinda Simon Msuva
ni vigumu kwa benchi la ufundi kumfikiria kumrejesha Shamte.
|
No comments:
Post a Comment