PAPISS
CISSE amefikia makubaliano na Newcastle kuvaa jezi mpya za klabu hiyo
zilizo na nembo ya mdhamini mpya ambaye biashara yake inaenda kinyume na
maadili ya imani ya dini ya mchezaji huyo.
Mchezaji
huyo mwenye miaka 28 alikataa kuvaa jezi zenye nembo ya kampuni ya
mikopo ya Wonga - kwa sababu kampuni hiyo inatoa mikopo yenye riba -
kitu ambacho hakiendani na imani ya dini ya kiislamu.
Alijitoa
kwenye ziara ya Newcastle ya kujiandaa na msimu mpya baada ya kusema
hana mpango wa kuvaa jezi zenye kupromoti kampuni inayotoa mikopo ya
riba lakini baada ya mazungumoz ya muda wa wiki kadhaa sasa jambo hilo
limepatiwa ufumbuzi.
Cisse amekuwa akifanya mazoezi peke yake
wakati wachezaji wenzake wakiwa nchini Ureno kwenye kambi ya pre season,
ingawa sasa anategemewa kujiunga nao mara moja.
Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote rasmi kutoka Newcastle kuhusu suala hilo.
|
No comments:
Post a Comment