Star wa NBA Lebron
James huenda asiichezee tena timu ya taifa ya Marekani kwenye michuano
mbalimbali ya kimataifa ambapo taarifa iliyotoka kwa walio karibu nae
mkali huyu wa Miami Heat ambayo mwezi uliopita aliiongoza kutwaa ubingwa
wake wa tatu wa NBA, ni kwamba amechoshwa na kucheza mechi nyingi za
timu yake ya NBA na timu ya taifa hivyo wakati timu ya taifa ikicheza,
yeye atakuwa karibu zaidi na familia yake.
L23 kama lilivyo jina
lake, ana familia changa ambayo anahitaji kuwa karibu nayo na anahisi
kuwa hakuna ulazima wa yeye kuwepo kuisaidia timu ya taifa kwani kuna
wachezaji wengine wanaoweza kujaza nafasi yake.
No comments:
Post a Comment