AC Milan ya Italia kwa mara ya kumi na moja katika
muda wa miaka kumi na mbili iliyopita imefuzu kushiriki Kombe la Klabu
Bingwa baranai Ulaya.
Milan imeilaza PSV Eindhoven kutoka Uholanzi kwa mabao 3-0.
Baada
ya kutoka sare ya 1-1 na Uholanzi katika mechi ya awamu ya kwanza,
Kevin Prince alifunga mabao mawili yaliyoiweka timu yake mbele, naye
Mario Balotelli akaongezea la tatu na hivyo kuihakikishia mabingwa wa
zamani wa kombe hilo nafasi katika raundi ijayo kwa jumla ya mgoli 4-1.
Katika matokeo mengine iliyochezwa siku ya
jumatano, Zenit St Petersburg iliikwaruza Pacos Ferreira kwa mabao manne
kwa mawili na kufuzu kwa hatua ijayo kwa jumla magoli manane kwa
matatu.
Kwingineko, mabingwa wa Jamhuri ya Czech,
Viktoria Plzen walishinda wenyeji wao Slovenia Maribor kwa bao moja kwa
bila na kujikatia tikiti ya raundi ijayo ya makundi ya kinyang'anyiro
cha kuwania Kombe la Klabu Bingwa Barani Ulaya.
Viktoria Plzen imesonga mbele na jumla la magoli 4-1.
Klabu hizo zitajiunga na Arsenal Schalke, Steaua
Bucharest na Austria Vienna ambazo zote zilishinda mechi zao siku ya
Jumanne katika hatua ya makundi. |
No comments:
Post a Comment