Mchezaji
mmoja wa Kimataifa wa Morocco, ambaye alikuwa amepigwa marufuku na
shirikisho la mchezo wa soka duniani, FIFA, amepatikana na hatia ya
kutumia madawa ya kusisimua misuli.
Mchezaji huyo ambaye jina lake halijatolewa,
alikuwa amepigwa marufuku ya kutocheza kwa siku thelathini na hatua
zaidi za kinidhamu imeanzishwa dhidi yake.
FIFA
imsema, marufuku hiyo inahusiana na kosa la kutumia dawa hizo
zilizoharamishwa baada ya mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia tarehe nane
mwezi Juni mwaka huu.
Baada ya kupokea matokea ya uchunguzi wa awali,
mchezaji huyo aliiomba shirikisho hilo kurudia tena na matokeo yake
yamekuwa sawa.
Uamuzi huo uliochukuliwa na mwenyekiti wa kamati
ya nidhamu ya FIFA tayari umewasilishwa kwa shirikisho la mchezo wa
soka nchini Morocco.
Mchezaji huyo sasa ana hadi tarehe nne mwezi ujao kuijulisha FIFA ikiwa anataka kesi hiyo kusikilizwa upya.
Hata hivyo shirikisho la soka nchini Morocco
linatarajiwa kuwasilisha taarifa yake na ushahidi kwa FIFA kabla ya
tarehe kumi na moja mwezi ujao.
|
No comments:
Post a Comment