Klabu ya Tottenham huenda ikalazimika kumpiga faini
nyota wake anayesakwa na Real Madrid, Gareth Bale baada ya kukosa kufika
uwanja wa mazoezi kwa siku ya pili mfululizo.
Kocha wa Tottenham Andre Villas-Boas amesema Bale ni sharti kutimiza wajibu wake licha ya kuwa huenda akajiunga na Real Madrid.
Real wametangaza azma yao ya kumsajili mchezaji huyo kwa
kitita cha pauni milioni 86, kiasi ambacho ndicho kubwa
zaidi duniani kwa klabu yoyote kumnunua mchezaji mmoja.
Bale, mweye umri wa miaka ishirini na minne,
alitarajiwa kurejea kambini siku ya Jumanne baada ya timu hiyo kwenda
likizoni katika eneo la Marbella.
''Kwa sasa Real inataka kumsajili Bale, ikiwa
hilo litatokea tunamtakia kila la heri, lakini kwa kuwa hajafika
kambini, hilo ni kosa na sharti airekebishe'' Alisema Villas-Boas.
Bale amehusishwa na klabu ya Real na kocha huyo wa Tottenham anasema usajili huo huenda ukakamilika hivi karibuni.
Klabu ya Tottenham haitaki kumuuza mchezaji huyo hadi pale watakapomsajili atakayechukua nafasi yake.
Ripoti zinasema Tottenham huenda ikamsajili mshambulizi wa klabu ya Roma kutoka Argentina Erik Lamela kuchukua mahala pa Bale.
Bale hajaichezea klabu ya Tottenham au timu ya
taifa ya Wales msimu huu kutokana na Jeraha, lakini mapema siku ya
Jumatano alitajwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Wales itakayocheza
mechi ya kufuzu ya kombe la dunia dhidi ya Macedonia na Serbia baadaye
mwezi huu. |
No comments:
Post a Comment