Aaron Ramsey alifunga mabao mawili na kuipa klabu
yake Arsenal ushindi wa wazi bila upinzani mkali dhidi ya Fenerbahce ya
Uturuki.
Katika mechi iliyochezwa hapo jana kwenye uwanja
wa Emirates, Arsenal imefuzu kwa Ligi ya Mabingwa kwa mwaka wa kumi na
sita mfululizo.
Wageni Fenerbahce walibaki nyuma
tangu mechi ya awamu ya kwanza walipofungwa mabao matatu kwa bila na
Arsenal. Adhabu hiyo kwa Fenerbahce imerahisisha kazi ya shirika la
kandanda la Uropa, UEFA, kwani sasa haitajishughulisha kuizuia klabu
hiyo kutoshiriki mechi ya ligi za mabingwa, hii inafuatia marufuku ya
miaka miwili ambayo inafaa kutolewa kwa Fenerbahce baada ya kushtumiwa
na hatia ya kupanga mechi.
Ikiwa klabu hiyo ingefaulu kushiriki Ligi ya
Mabingwa basi kingekuwa kibarua kigumu kwa UEFA kutekeleza sheria na
adhabu ipasavyo.
Hii leo jumatano, mahakama ya rufaa itasikiliza kesi hiyo.
Arsenal imewahi kushindwa na timu za Uropa mara
mbili tu katika muda wa miaka hamsini, huku klabu hiyo ya Uturuki
imepata kufunga mabao mara tatu tu katika ziara zake nane za England. |
No comments:
Post a Comment