Klabu ya soka ya Uturuki, Fenerbahce, imepigwa
marufuku ya kushiriki katika michuano ya bara Ulaya msimu huu, baada ya
mahakama ya upatanishi ya michezo CAS, kuidhinisha uamuzi uliokuwa
umetolewa na shirikisho la UEFA kuwa klabu hiyo ilihusika na sakata ya
kupanga matokeo ya mechi.
Klabu hiyo ilikuwa, tayari kujiunga na ligi hiyo
ya daraja ya pili, baada ya kuondolewa na Arsenal katika michuano ya
kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya.
Shirikisho la UEFA, liliipiga marufuku
Fenerbahce mwezi Juni mwaka huu, baada ya kuwapata maafisa wa klabu hiyo
na hatia ya kupanga matokeo ya mechi ili kushinda ligi kuu ya soka
nchini Uturuki. |
No comments:
Post a Comment