Hasira za Yanga kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Wagosi wa Kaya
Coastal Union zimeishia kwenye basi la Wagosi hao wa Kaya baada ya
mashabiki kuamua kulipopoa mawe.
Tukio hilo limetokea nyuma ya uwanja wa Taifa wakati basi lililobeba
wachezaji na viongozi wa Coastal Union lilipokuwa likiondoka uwanjani
hapo.
Mashabiki waliokuwa wamebeba mawe walianza kulishambulia basi hilo la
Coastal na kupasua vioo ambavyo vimemuuza beki wa pembeni Ahmad Juma
aliyechanika sehemu ya nyuma ya kichwa.
Hilo ni tukio la pili mfululizo kwa Coastal Union kushambuliwa na
mashabiki wa Yanga,kama itakumbukwa msimu uliopita pia mashabiki wa
Yanga waliwahi kuishambulia timu hiyo ya kutokea huko Tanga.
Mkurugenzi wa ufundi wa Coastal Union Nassor Binslum akizungumza na
Supermariotz amelaani kitendo hicho akisema si kitendo cha uwanamichezo
na kinapaswa kulaaniwa na kila mpenda soka.
Kwenye mchezo huo goli la Yanga limefungwa na Didier Kavumbagu wakati
lile la Coastal Union likiwekwa wavuni kwa penati na nahodha Jerry
Santo.
Mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoro aliyevurunda katika mchezo huo
alitoa kadi nyekundu kwa Crispin Odula wa Coastal Union na Simon Msuva
wa Yanga.
Katika michezo mingine iliyochezwa leo Simba wamepata ushindi wa bao 1-0
dhidi ya JKT Oljoro kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid bao likifungwa
na Harun Chanongo.
Huko Tabora kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Azam FC wamechomoza na
ushindi wa mabao 2-0 yakifungwa na Gaudance Mwaikimba na Seif Karihe.
Uwanja wa Sokoine Mbeya City wamewafunga maafande wa Ruvu Shooting 2-1
wakati huko Mkwakwani Mgambo JKT wamewachapa Ashanti United 1-0.
|
No comments:
Post a Comment