Kiungo mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Gareth Bale hapo jana
aliwaaga rasmi wachezaji wenzie ikiwa ni ishara ya kukaribia kwake
kuihama klabu hiyo kujiunga na Real Madrid .
Bale aliwaaga wachezaji wa Spurs kwa kutia saini za kumbukumbu kwenye
jezi zao walipokuwa wanapanda ndege kuelekea nchini Ufaransa ambako
watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Monaco .

Bale alibaki nyuma jijini London ambako anamalizia sehemu za mwisho
za mazungumzo ya uhamisho wake kwenda klabu ya Real Madrid ambayo
imekuwa ikimfanya juhudi za kumsajili .
Gareth Bale anatarajiwa kukamilisha usajili huo ndani ya siku chache
zijazo na inaaminika kuwa Madrid watalipa ada ya uhamisho ambayo
itavunja rekodi ya usajili .
|
No comments:
Post a Comment